NA ABDI SULEIMAN.
MENEJA Kitendo cha Maradhi yasioambukiza Zanzibar (NCD) Dr.Omar Mohamed Suleiman, amesema maradhi ya NCD ni mengi katika jamii, hivyo waandishi wa habari wanapaswa kujitoa kwa dhati kuelimisha jamii juu ya uwepo na madhara ya maradhi hayo.
Alisema waandishi ni kiungumo muhimu sana katika jamii, kwani kalamu na sauti zao zinakubalika kama ilivyo kwa wanasiasa, hivyo wakitumia taalamu zao kwa kuandika, kutangaza na kuripoti juu ya maradhi hayo jamii itaweza kuchukua tahadhari sana.
Meneja huyo aliyaeleza hayo wakati alipokua akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari, wakati wa mafunzo ya maradhi ya NCD yalioandaliwa na kitengo hicho na kufanyika mjini Chake Chake.
“Mradhi haya ni mengi sana huwezi kumjuwa mgonjwa wenye NCD kwa kumuona kwa macho, vizuri tukawaelimisha wananchi wetu maradhi haya yanapoteza watu kuliko maradhi mengine,”alisema.
Alisema kutoka na hali hiyo hakuna aliyesahihi ikiwa ni kisukari, presha, shinikizo la damu, ili kupunguza ongezeko la wagonjwa ni lazima kufanywa uhamaisishaji kwa kutumia mabonanza na wataalamu wa NCD wataweza kutoa taalamu na kupima.
Aidha aliwataka wananchi kutumia matunda kwa wingi katika ulaji wa vyakula vyao, ili kupunguza maradhi mengi mwilini ikiwemo na gesi, pamoja na wananchi kwenda hospitali kuchunguza afya zao.
Nae mratib wa Kitengo cha NCD Pemba Dr.Haji Khatib Fakihi, aliwashauri wananchi kuendelea kufanya kazi za majumbani na kuzichukulia kama ni fursa ya kupunguza unene na kufanya mazoezi.
Kwa upande wake msaidizi Mratib wa NCD Pemba Dr.Hussan Suleiman Juma, akiwasilisha mada katika mkutano huo aliwataka akinamama kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara, ili kujua afya zao pamoja na kuzuwia saratani ya shingo ya kizazi.
Akizungumzia suala ulaji wa vyakula, aliwataka waandishi kuhamasisha jamii kula mlo kamili wenye makundi mbali mbali ya chakula, ikiwemo nafaka/mizizi/ndizi, matunda, mbogamboga, jamii ya kunde, asili ya wanyama.
Alisema ipaswa kupunguza kutumia vyakula vyenye mafuta mengi, tumia mafuta kijiko cha kulia chakula wakati wa kupika chakula cha familia ya watu wanne, pamoja na kuepuka matumizi makubwa ya chumvi isizidi kijiko kimoja cha chai kwa siku kwa familia ya watu wane.
Kwa upande wao waandishi wa habari wameahidi kufanyia kazi mafunzo hayo, kwa kuhakikisha wanaisaidia jamii, katika kuepukana na ulaji wa vyakula bila ya mpangilio.
Walisema watajitahidi kutumia nafasi yao kutoa elimu juu ya maradhi ya NCD kwa lengo la kupunguza wananchi kutumbukia katika maradhi ya NCD.
MWISHO