NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
VIJANA Kisiwani Pemba, wameshauriwa kuchangamkia fursa za utengenezaji wa pegi za plasiki za kupandia mwani, ili kupunguza uharibifu wa mazingira kwa ukataji wa miti wakati wa kupanda zao.
Wakulima mwani hutumia pegi za miti wakati wakupanda zao hilo, hali inayopelekea uharibifu wamazingira kwa kukata miti katika maeneo yaliyokaribu na bahari.
Alisema mwani umeajiri wananchi wengi na wote wanatumia majiti wakati waupandaji wa mwani, hivyo juhudi za makusudi zinahitajika kunusuru uharibifu wa mazingira.
“Sisi tumeshajihishana ndani ya mwaka huu tumeweza kupanda miti zaidi ya 6000 za mikandaa, katika maeneo yaliyowazi ili kupunguza kasi ya maji kuingia katika kisiwa chetu, timi mingi ilikatwa kwa shuhuli mbali mbali,”alisema.
Nae Hamadi Kombo Omra mkaazi wa mpambani Kojani, alisema kama wakulima wa mwani wataendelea kukata miti, basi itafika wakati kisiwa na maeneo mengina yatakua jangwa.
Aidha aliwataka wakulima hao kuhakikisha wanakua mstari wambele katika upandaji wa miti, ikizingatiwa wao ndio wakataji wakubwa wa miti.
“Serikali na makampuni yanayonunua mwani, kuwapatia vifaa mbadala za kupandia mwani, ili waweze kuachana na utumiaji wa miti ambayo pia hupelekea kuharibu mazingira ya bahari baada ya kuoza,”alisema.
Kwa upande wake mkulima wa mwani katika eneo la likoni Kojani Haji Juma Ali, alisema baada ya kukosa pegi mbadala wanalazimika kutumia pegi za miti, ili kupandia mwani wao ambao haukokoti na maji.
Alisema wanapotumia miti mwani unatulia vizuri baharini wala haukokotwi na maji, hivyo aliyomba serikali kupatia vitu mbadala ambavyo wanaweza kutumia wakati waupandaji wa mwani.
Afisa Mdhamini Wizara ya Uchumi wa buluu na Uvuvi Pemba Dr.Salim Mohamed Hamza, alisema tayari wakulima wa mwani Pemba wameshapitiwa elimu juu ya kupanda mwani kwa kutumia Plastiki, Nanga ili kunusuru uharibifu wamazingira kwa ukataji wa miti.
“Tayari wakulima wa mwani Makangale, Tumbe, kojani wote wameshapatiwa elimu juu ya kutumia malighafi nyengine wakati wa kupanda mwani na ukastawi vizuri pia,”alisema.
Aidha mdhamini huyo aliwataka wakulima wa mwani Kisiwani hapa, kuwa mstari wambele katika suala la uhifadhi ya mazingira kwa kuachana na ukataji wa miti, badala yake kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kupanda miti.
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) John Chikomo, alisema JET imekua mstari wa mbele katika kushajihisha wananchi kutunza, kuhifadhi na kulinda mazingira.
alisema kwa sasa JET inatekeleza mradi wa tuhifadhi Maliasili unaofadhiliwa na USAID, jukumu la uhifadhi wa mazingira ni wananchi wote, hivyo wakulima wa mwani wanapaswa kuwa mstari wambele katika suala zima la utunzaji wamazingira kwa kuachana na ukataji wamiti.
Kwa mujibu wa bajeti ya waziri ya Uchumi wa buluu na Uvuvi Zanzibar 2023/2024 imesema uzalishaji wa zao la mwani umeongezeka kutoka tani 10,531 mwaka 2021 hadi tani 12,594 kwa mwaka 2022, ambapo usafirishaji wa mwani nje ya nchi umeongezeka kutoka tani 12,124 mwaka 2021 hadi tani 13,972 mwaka 2022.
Huku Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamius, katika bajeti ya Wizara yake 2023/2024 alisema, mazao ya misiti takwimu zinaonyesha mwaka 2022 matiumizi ya kuni yameongezaka kutoka mita za ujazo 25,813 mwaka 2021 hadi kufikia mita za ujazo 26,236.
Kwa upande mkutano wa COP26 kilele wa wiki mbili huko Glasgow, umesema karibu hekta milioni 12 ya misitu katika dunia ya kitropiki ilipotea mwaka 2018, sawa na kupoteza viwanja 30 vya mpira wa miguu kwa dakika.
Kwa mujibu wa Sensa ya wakulima wa mwani, iliyofanywa na Idara ya mazao ya baharini Pemba 2020 Pemba iina jumla ya wakulima wa mwani 18000, huku wanawake wakiwa zaidi ya asilimia 80.
MWISHO