Monday, November 25

UTPC yawapatia mafunzo waandishi wa habari namna ya kuandika habari za usawa wa kijinsia.

NA FATMA HAMAD FAKI – MOROGORO.

Wandishi wa habari wametakiwa kuendelea kuibua kero zinazo wakabili wanawake na kuzisemea ili waweze kupata fursa mbali mbali za kimaendeleo zilizopo Nchini.

Wito huo umetolewa  na Mkurugenzi wa umoja wa vilabu vya wandishi wa wandishi wa habar Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wandishi wa vyombo mbali mbali vya habari Tanzania yanayohusu usawa wa kijinsia yaliyofanyika Flomi Hotel Morogoro.

Alisema wandishi wa habari wanamchango mkubwa katika kufikisha ujumbe kwa jamii, hivyo ni vyema kutoa elimu kwa jamii,  kutatua changamoto zilizopo.

“Ndugu zangu wandishi wa habar mtakapoibua kero za wanawake na kuzisemea mtaweza kuleta  mabadiliko kwa wanawake hao” alisema Mkurugenzi.

Aidha Mkurugenzi huyo amewata wandishi waliopatiwa mafunzo hayo kuyatumia vyema kwa kuandika habarI zinazohusu usawa wa kijinsia ili kuleta mabadiliko katika jamii hususani kwa wanawake.

Mapema msimamizi wa masuala ya kijinsia kutoka UTPC Hilda Kileo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habar kuandika habari kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshwaji wanawake katika nyanja tofauti ikiwemo kiuchumi na siasa.

Akiwasilisha mada mkufunzi wa mafunzo hayo Deo Tembo alisema endapo kutakua na uwasa wa kijinsia katika nyanja mbali mbali kutakuza uchumi na kuwafanya wanawake kupiga hatua kimaendeleo.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru kwa kupata mafunzo  hayo huku wakiahidi kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko kwenye jamii.

Mafunzo hayo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wandishi wa habar yameandaliwa na UTPC chini ya ufadhili wa ubalozi wa Sweden.