NA OMAR HASSAN/SAID BAKAR – ZANZIBAR
Kamishna wa Polisi Zanzibar HAMAD KHAMIS HAMAD amesema kuheshimu na kulinda haki za binaadamu na kulinda utu wa kila mtu kwa Askari Polisi sio tu ni wajibu wa kisheria bali ni sharti la kimaadili katika taaluma ya Polisi.
Akifungua mafunzo ya haki za Binadamu kwa Askari wa Mikoa mitatu ya Unguja huko Ukumbi wa Chuo cha Polisi Zanzibar amesema lazima askari afanye kazi kwa karibu na raia kwa kuwa na huruma, kutonyanyasa, kulinda makundi yaliyo katika mazingira hatarishi na kuzingatia uadilifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuia ya kukabiliana na changamoto za vijana Zanzibar (ZAFAYCO) amesemema kuimarisha mfumo wa haki jinai na kupunguza vitendo vya uvunjifu wa haki za binaadamu kunaenda sambamba na kuimarisha uchumi.