NA KHADIJA KOMBO- PEMBA.
Wazazi na walezi nchini wameshauriwa kutenga muda wa kuwa karibu na Watoto wao ili waweze kuzungumza nao mambo mbali mbali yanayohusu makuzi yao.
Akifungua mjadala juu ya kujadili changamoto zinazo wahusu Watoto kwa wazazi, walezi Pamoja na wadau wengine wa Watoto huko katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Chake Chake Mrajis wa asasi za kiraiya Pemba Ashrak Abdalla Ali amesema hivi sasa wazazi na walezi wamekuwa wakijishughulisha na harakati zao za kujitafutia Maisha Zaidi na kukosa muda wa kukaa na Watoto wao na kujua matatizo yanayowakabili.
Kwa Upande wake Mongozaji wa mjadala huo Mratib Wa TAMWA Zanzibar kwa upande wa Pemba Fat-hiya Mussa Said amesema ni vyema wazazi na walezi kuhakikisha muda wote wanakuwa karibu na Watoto wao ili waweze kuwa salama wakati wote.
Kwa upande wao washiriki wa Mjadala huo wameshauri wazazi kuangalia namna ya kurudisha mfumo wa malezi ya pamoja ili kuwaweka watoto katika mazingira salama
Mjadala Huo ambao umewashikisha wanajamii, wanaharakati kutoka jumuiya tofauti zisizo za kiserikali, masheha Pamoja na waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali vilivyoko Kisiwani Pemba umeandaliwa na Umoja wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Pemba ( PACSO) chini ya ufadhili wa Irish Aid.
MWISHO.
ANGALIA VIDEO HII KWA KUBOFYA HAPO CHINI