Sunday, November 24

ALIENUSURU MAISHA NA UHAI WAKE KWA KUFANYA MAZOEZI PEMBA AWAASA WANAJAMII .

AMINA AHMED MOH’D-PEMBA.

“MAZOEZI NI AFYA” Ni Msemo ambao hutumika mara nyingi katika  Kuhamasisha  Mazoezi Ili Kuondokana na Maradhi Yasioambukiza Ikiwemo  Shinikizo la Damu Kwa Jina la kitaalamu (Pressure) Sukari, Ugonjwa Wa Moyo Kiharusi, Saratani na Mengi Mengineyo ambayo Yanaendelea kuchukua Roho za Watu Siku hadi Siku .

Inathibiti kwa Vitendo  Kauli hii Maarufu katika vinywa vya Watu wengi kufuatia kutengamaa kwa Afya ya Muhammed Ali Omar  Mkaazi Wa Gombani  Chake Chake ambae Amenusuru Maisha yake baada ya kuamua kufanya Mazoezi.
Mpendwa Msomaji leo Maalum  Mwandishi wa Makala hii Amezungumza na  Muhammed Ali Omar Umri  39 ambae Mkaazi wa Gombani Chake Chake  Kusini Pemba ambae Kutokana na kufanya Mazoezi ameweza  kuondokana na  Magonjwa Nyemelezi yasioambukiza  yaliokuwa Yakihatarisha Afya na Uhai wake.
” Mazoezi ndio Tiba Sahihi Kwa hali yangu ilivyokuwa mimi na Familia  yangu nilishajikubalisha kufanya Upasuaji (Operation) lakini kwa Sasa Akili za kufanyiwa Upasuaji Sizitaki Tena kabisa nimejikubalisha kufanya Mazoezi tu na nimekuwa Imara na nimepata nafuu Alhamdulillah “.
Kabla ya kuamua kufanya  Mazoezi  Alilazimika kufanyiwa Upasuaji huku Roho za Wanafamilia Zikikosa Matumaini kutokana na Afya yake Kuwa mbaya Siku hadi Siku ni baada ya  Kuvimba Mguu wake wa Kulia  na Kuthibitishiwa  katika Hospitali ya Muhimbili kuwa Uvimbe huo umetokana na  Ugonjwa wa Moyo ambao umepelekea Kuganda kwa Damu kutokana na kushuka kwa “Pressure ” Ugonjwa wa Shinikizo la Damu Ambao tayari Ulikuwa sugu Mwilini Mwake .
Mpendwa Msomaji wa Makala hii, Sinikizo la Damu  (Pressure)   ni Ugonjwa usioambukiza ambao umekuwa  ukiathiri  Zaidi hali za watu wenye Umri kati ya Miaka 25 hadi 65 Duniani kote.
Kabla ya  kujua Mengi kutoka kwa Muhammed Tuliangalie Suala hili la Shinikizo la Damu kitaalamu zaidi kutoka kwa Dakatari ambae Katika maisha yake Yote amekua akitoa hufuma kwa Wagonjwa wa Maradhi yasioambukiza Zanzibar.
 DALILI ZA SHINIKIZO LA DAMU ( PRESSURE)  NI ZIPI NA NINI MAANA YAKE! 
Omar Muhammed Suleiman ni Daktari  Mkuu Kutengo cha Maradhi yasioambukiza Zanzibar anasema kuwa  Zipo Atahari mbali mbali zinazotokana na  Ugonjwa wa Shinikizo la Damu  ikiwa ni Pamoja na Magonjwa ya Figo, Uharibifunwa Macho na kushindwa kuona, Kutanuka kwa Moyo, Shambulio La Moyo Heart (attach) Kiharusi, Magonjwa ya Moyo kama vile  Moyo kushindwa kufanya kazi  Pamoja na Kifo.
” Daktari  Omar Anasema Dalili kubwa za Ugonjwa wa  Shinikizo la Damu (Pressure) ni  Kuumwa na Kichwa, Kizungu zungu, Kichefu Chefu, au kutapika sana, Maumivu makali katika Ziwa la Kushoto, Uchovu mara kwa mara, Kuhisi Mapigo ya Moyo kwenda mbio, Kutokwa na Damu Puani, Uoni Hafifu,(Blurring if Vision) Pamoja na kupooza Sehemu ya Mwili.
KABLA YA KUFANYA MAZOEZI MUHAMMED ALIKUWA NA HALI GANI! 
” Tatizo langu ilikuwa ni Mguu wangu kuvimba, Damu ilibloki ,  Mishipa ya Moyo  Ilikuwa membamba  Hospitali walipokuwa wananicheki na kuniuliza, Vipi! Hauna homa za Mara kwa Mara   lakini Kwa vile nilikuwa napata kweli homa hizo niliwaambia  Hapa ndio mahala pake Kiasi ambacho Ile baridi Kidogo tu Mimi Siiwezi” Alisema Muhammed ambae  katika kuongea kwakwe imenilazimu kuweka Usawa juu ya  maneno aliyotamka ” Bloki” Aliyomaanisha Kuganda kwa Damu pamoja na ” kucheki” akiwa na maana ya kufanyiwa Uchunguzi.
“Dakatari Aliniandikia Dawa Pamoja na kunitaka nifanye kwa lazima Mazoezi ili kuweka Sawa  Pressure yangu “.
 “Yote Hayo yalitokana na  Mimi kuwa na Msongo wa mawazo uliosababishwa na  Changamoto ambayo Sitakuwa tayari kuiweka wazi ndugu  Mwandishi  lakini jamii ielewe kwamba chanzo cha Maradhi yangu yaliatokana na Msongo wa Mawazo” .
 ” Huwezi kuamini Tangu nilipoanza Mazoezi zile homa za mara kwa mara Zimekimbia Zote, Na Mguu ulikiwa unaniuma vibaya Sana kiasi ambacho siwezi kutembea wala lakini saivi Nashukuru Alhmdulillah nafanya safari Zangu naweza Kutembea kilo mita Tano kwa Saa Moja mpka Kilomita 6 jambo ambalo awali nilikuwa siwezi kabisa kufanya ivo” Alisema .
 “Upasuaji mambo ya Mishipa ya miguu unajua tena Roho zikiwa na wasi wasi na hofu kidogo mara yanajitokeza Mengine, Wenzanhu Walifanyiwa uoasuaji wale ambao nilikuwa nao  kliniki Muhimbili pamoja lakini mimi Baada ya kufata ushauri wa Dakatari nimeamua kama ni Mpangilio wangu wa Kila Siku Lazima nifanye Mazoezi “.
 Muhammed Anasema Nafuu ya Moja kwa Moja katika kurudisha mwili wake Katika Hali ya kawaida  ilianza kidogo kidogo kutoka Mwaka 2018 ambapo alianza kufuata ushauri wa Dakatari kufanya Mazoezi  hadi  Kuimarika Mnamo mwaka 2020.
JEE! WANAOMJUA MUHAMMED WANAZUNGUMZIAJE MUHAMMED AWALI NA SASA HIVI!. 

Fatma Ali Muhammed na Sadamu  Ali Mbarouk  ni Miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakiungana pamoja katika kufanya  Mazoezi  kila Siku na Muhammed katika kikundi cha Mazoezi ya Viungo Gombani Fitness Club wanasema  kuna mabadiliko makubwa ya kiafya wanayoyaona  kutoka Awali alivyoanza kufanya Mazoezi  hadi Sasa.

“Alipokuja Binafsi nilikuwa naogopa kutokana na Mguu wake ulivyokuwa Sikuweza kumuangalia mara Mbili kwa Sababu nilikuwa nahofia sana nilihisi kama anajiumiza vile lakini siku zilivyozidi niliweza kuona anabadilika  nikamuhisi yupo kawaida.” Alisema Fatma Ali

 HALI YA UGONJWA IPOJE?! 
 Tatizo hili la Magonjwa  yasioambukiza  kwa Jina la kitaalamu( Non Comunicable Diseases) (NCDs) yanachangia Takribani Asilimia 33 ya vifo vyote nchini huku Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO)zikionesha kuwa  kwa mwaka 2020 zilionesha kuwa Magonjwa hayo yalichangia zaidi ya Vifo Milioni 41 sawa na asilimia 71 ya vifo vyote Duniani ukilinganisha na vifo milioni 57 kwa mwaka 2016 Duniani.

Aidha kwa Mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Waziri Wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui  wakati wa  Uzinduzi wa Utafiti wa Kitaifa wa Viashiria vya Magonjwa Yasiyoambukiza (STEPS SURVEY 2023) uliofanyika  katika  Ukumbi wa Tawimu Jijini Dodoma     alisema kuwa  Tatizo la Ugonjwa wa sinikizo la Damu (Pressure) kwa sasa  limeongezeka   ukilinganisha na Miaka iliyopita pamoja na  Magonjwa mengine yasioambukiza ikiwemo kisukari  pamoja na Magonjwa ya Mfumo wa hewa.

“Takwimu hizo zote kutoka katika Vituo vyetu vya kutolea Huduma za Afya Nchini zinaonesha ongezeko kubwa sana la Magonjwa hayo ambapo katika Kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023, Magonjwa yasiyoambukiza ambayo yalisababisha Wagonjwa wengi kuhudhuria Vituo vya Huduma za Afya ni Pamoja na Shinikizo la juu la Damu Wagonjwa 1,456,881 sawa na Asilimia 49 ukilinganisha na Asilimia 34 kipindi kama hicho Mwaka 2021/2022 ,Kisukari Wagonjwa 713,057 sawa na asilimia 24, Magonjwa ya Mfumo wa hewa Wagonjwa 386,018 sawa na asilimia 13 ikilinganishwa na Asilimia 10 kwa Kipindi kama hicho Mwaka 2021/2022.

 MUHAMMED ANA WITO GANI  KWA WANANCHI WENZAKE!

Muhammed Amewaasaa Wananchi Wote  Unguja na Pemba kutenga Muda maalum kufanya Mazoezi  Kuimarisha Afya zao na kuondokana na maradhi Nyemelezi ambayo yanasababishwa  na sababu mbali mbali ikiwemo Msongo wa Mawazo, Ulaji usiofaa, Uzito wa kupitiliza   Ulevi na vyanzo  vyengine mbali mbali.
” Dhana ya Mazoezi ni Afya inatendeka tu kwa Mdomo lakini kuna wimbi kubwa bado hawaifanyii kazi niwaase Wazaznibari wenzangu wanwake na wanaume vijana na watoto  Kutenga mda hata wa Dakika 30 tu Kwa Siku kufanya Mazoezi  ya Aina yeyote ikiwa kukimbia kuruka ruka kunyoosha viungo na mengine yote kuweka Sawa Afya Zetu “.

Muhammed Alimalizia kwa kusema kuwa Kinga ni Bora kuliko Tiba hivyo haitokuwa vyema kusubiria Tiba wakati Kujikinga na Maradhi yasioambukiza ni jambo linalowezekana.

MTAALAMU WA AFYA NAE ANATOA WITO GANI JUU YA SUALA HILI!

Dokta Omar amewataka Wananchi Unguja na Pemba Na duniani kote amewataka Wananchi kuendelea kuchukua hatua Ili kuweza kujiepusha na Ugonjwa wa Shinikizo la Damu  ikiwa ni Pamoja na kufanya Mazoezi ya Viungo kila Siku, Kuepuka kula vyakula vyenye Mafuta mengi ambaoo amesema mwili, unahitaji mafuta kwa kiwango kidogo kisichozidi nusu kijiko  kwa Siku, kuepuka kutumia Mafuta ya Wanyama sambamba na kula Nyama Nyekundu kwa wingi, Kupeka Matumizi ya Pombe, Kudhibiti Msongo wa Mawazo, kudhibiti Uzito wa kupitiliza  Uzito kuendana na kimo cha mwili , Kula Mlo kamili, Mboga mbiga na Matunda  Kuepuka amatumizi ya  Chumvi.

Aidha Dokta Omar amewaasa wananchi kujenga Tabia ya kuchunguza Afya Zao mara kwa mara ili kuweza kubaini Changamoto mbali mbali za Kiafya.

Ikiwa  Muhammed Ameamua kubadilisha Afya na  Maisha yake  kwa kufanya Mazoezi na kuepukana na Maradhi Nyemelezi homa za mara kwa mara pamoja na kuimarisha Afya yake kwa kufanya Mazoezi  bila Shaka  Msomaji unaweza Kubadilika kuamzia sasa kwa kutenga muda Kufanya Mazoezi kupekana na Maradhi Yasioambukiza.

Mwisho.