PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.
Na Rahma Khamis – Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara inaendelea kuchukuwa juhudi za kuhakikisha Hospitali zote zinaanza kutoa huduma za Mfuko wa huduma ya Afya kwa Wanannchi ifikapo mwezi Octobar mwka huu.
Akifunga mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo watendaji wa Mfuko huo na wadau wa maendeleo huko katika Ukumbi wa Zura Maisara amesema kupitia huduma hiyo Wizara itahakikisha inatoa huduma bora za Afya kwa jamii na kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi hao.
Aidha alieleza kuwa Serikali itashirikiana na wadau wa maendeleo katika kufankisha upatikanaji wa huduma bora za Afya kupitia Mfuko huo.
Hata hivyo amesema Serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa wananchi wake wanakua na afya bora ili kuweza kushiriki katika harakati za ujenzi wa Taifa.
Aidha Waziri amefahamisha kuwa adhma ya Serikali ya awamu ya nane chini uongozi wake Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kuhakikisha wananachi wote wanapata huduma bora za afya bila ya kujali hali zao za kifedha.
“Muheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi ,Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amefanya ujasiri wa kuanzisha Mfuko wa huduma za Afya hivyo hakuna budi kumuunga mkono kwa hali na mali,”alikumbusha Waziri.
Ameongeza kuwa Zanzibar imechagua mpango wa Bima ya Afya kwa wote (Universal Health Insuarence Scheme) kama utaratibu wa ufadhili wa UHC ambao utagharamiwa kwa kodi ya jumla,michango ya wananchama na msaada kutoka kwa washirika wa maendeleo.
Waziri alisema kuwa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya fedha na Mipango itatoa msaada unaohitajika kuhakikisha mpango wa Universal Health Insuarence unafanikiwa na kutumika nchini.
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kujiunga katika Mfuko wa Hudma za Afya ili kupunguza usumbumbufu wanaoupata wakati wanapopata matatizo ya kiafya.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Mbarouk Omari Moh’d amesema mfuko huo ni mpya hivyo kunaweza kujitokeza changamoto mbalimbali hakuna budi kushirikiana na wadau wengineili kuweza kupata mipango na mawazo yao yatakayoweza kusaidia kuimarisha mfuko huo.
Aidha amefahamisha kuwa Serikali inategemea kupata fedha kutoka kwa wadau,wafadhili pamoja na wananchi wenyewe waliojiunga kuwezesha mfuko huo kuwa endelevu.
Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya fedha za nje Yussuf Ibrahim Yussuf amesema wamejipanga kuhakikisha fedha zinazotarajiwa kutumika katika mfuko huo zinapatikana kwa wakati uliopangwa.
Aidha amesema ushirikiano uliopo kati ya Ujerumani na Zanzibar ni hatua moja ya kuleta maendeleo katika kuinua na kuimarisha maisha ya wazanzibar.
Warsha hiyo yenye lengo la kuimarisha Mfuko wa Hudma za Afya Zanzibar imeandaliwa na Mfuko wa Afya chini ya ufadhili wa Wadau kutoka Ujerumani na Swizland.