
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab, amewataka wajumbe wa kamati tendaji ya ZFF Kisiwani Pemba, kutambua thamani yao katika kuendeleza na kuinua mpira wa Kisiwa cha Pemba na Zanzibar.
Alisema iwapo wajumbe hawatakua kitu kimoja, kuachana na fitna, majungu, kufanya kazi kwa kutafuta mbinu na kuona wapi wanaweza kupata fedha na kuinua mpira ndani ya kisiwa hicho.
Aidha alisema iwapo watakua kitu kimoja basi hatotokea mtu yoyote kuwatinia fitna au kuwafitinisha, baada ya kuwa na msomamo mmoja wa kuendeleza soka la Zanzibar.
“Kama mutakua kitu kimoja kwa kila jambo, basi maduwi wanaowafitinisha hawatapata nafasi pale mutakapokuwa wazazi na kuweka ukweli wote,”alisema.
Katibu Mkuu huyo aliyaeleza hayo katika mkutano wa pamoja baina ya wajumbe wa kamati Tendaji ZFF upande wa Pemba, alipofika kusikiliza changamoto za wajumbe wa kamati hiyo.
Alisema ZFF imepata rais Rais makini na mzuri na kuhakikisha wanakaa pamoja na kuondosha tafauti zilizopo kwa kuhakikisha migogoro iliyopo inaondoka kabisa.
Hata hivyo aliwashauri wajumbe hao kukaa na viongozi wao wa majimbo, ili kuona wanasaidia vipi michezo kwani viongozi wa majimbo Unguja, wanasaidia timu zao na kuona zinafanya vizuri katika mashindano mbali mbali ya ndondo.
Nae Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Mfamau Lali Mfamau, aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kuwa na umoja, mshikamano, mashirikiano na kuachana na unafiki baina yao ili kuhakikisha wanaendeleza mpira wa Zanzibar.
Hata hivyo aliwataka wajumbe hao kuhakikisha wanasimamia ipasavyo sheria na kanuni za mashindano hayo, kwani taratibu zilizopo zinatekelezwa ipasavyo.
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati hiyo Yahya Khami Ali, alisema mashirikiano ndio jambo litakaloufikisha mbele mpira wa Zanzibar, ambapo kwa wasasa wamekosa ushirikishwaji kutoka kwa viongozi wajuu wa ZFF.
Alisema ZFF haiwezi kitekeleza majukumu yake bila ya wajumbe wa kamati tendaji kupata taarifa, vitu ambavyo vinafanywa bila ya kushirikishwa wajumbe wa Pemba, ikiwemo kutolewa kwa kanunu ya mashindano, Raita ya ligi msimu 2023/2024, hivyo ipo haja wizara kuwakutanisha viongozi wa ZFF unguja na Pemba.
Hata hivyo alimshukuru Rais wa Zanzibar kupitia Wizara ya Habari, kuufanyia matengenezo makubwa uwanja wa michezo Gombani ambao sasa utaweza kutumika hata michezo ya usiku.
“Wajumbe wa kamati tendaji walikuja Pemba, kutembelea viwanja vya michezo na kuupitisha uwanja wa kishendeni kutumika kwa ligi, uwanja ambao haufai kufuatia kuwa na mawe mengi,”alisema.
Nae Ali Mohamed Ali Mjumbe kamati tendaji ZFF, alisema yote yanayotokea ni kutoka na katibu Mkuu wa ZFF kuwa ndio kikwazo mkubwa kwa kutokuwashirikisha ipasavyo wajumbe wa Pemba.
“Haiwezekani unamwambia mtu saa tano asafiri, wakati taarifa ya safari ipo mwezi mzima, yote ni kutokana na kutokuwa na maelewanao na wajumbe wake wa Pemba,”alisema.

Alisema bado wanania njema na mpira wa Zanzibar, ili kuona soka lina kuwa na kufikia malengo yao, ila mashirikiano ndio kitu cha msingi na kuona wanapiga hatua kimaendelkeo.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Omar Ahmed Awadhi, alisema bado katika utendaji wa ZFF hakuko sawa na kuna tataizo kubwa Pemba kuna wajumbe watano lakini wanashindwa kushirikishwa ipasavyo na viongozi wenzao wa Unguja.
Alisema umoja mshikamano ndio utakaopelekea mpira wa Zanizbar kurudi katika hadhi yake na kutambulikwa kama ilivyokua katika miaka ya nyuma.
Makamu wa Rais wa ZFF Abdalla Yahya Shamuuni, alisema suala la katibu mkuu wa ZFF bado Wizara ya Habari haijataka kulifanyia kazi, kwani inaweza kuliingilia kwa maslahi ya mpira wa miguu.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa ZFF na Vilabu kuheshimu kanuni za kuendelea mpira wa miguu pale maamuzi yanapotolewa kwa maslahi ya mpira wa Zanzibar.
Nae naibu katibu Mkuu ZFF Khamis Hamad Juma, aliomba wizara kuwapatia mkufunzi wa waamuzi katika kisiwa cha Pemba, kwa lengo la kuwafunza waamuzi vijana juu ya kujua sheria mbali mbali mpira wamiguu.
MWISHO
Abdi Juma Suleiman