NA FATMA HAMAD PEMBA,
Vijana wameonywa kuepuka kukaa katika vigenge viovu ,na badala yake wajiunge na vikundi vya ushirika, ili waweze kujipatia kipato cha halali.
Ushauri huo umetolewa na katibu wa kikundi cha ushirika mapambano cooperative kinacho jishuhulisha na ufugaji wa Samaki, kaa, kamba na mboga mboga Bishara Muhammed Mussa mbele ya wanakikundi hao, mara baada ya kutembelewa na wajumbe kutoka wizara ya uchumi wa Buluu na shirika la IUCN kutoka Tanzania bara huko Sizini wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazi Pemba.
Alisema wakati umefika kwa vijana kuwamka na kujiajiri wenyewe, na sio kukaa tu vigengeni na kusubiri ajira Serikalini.
‘’Vijana mtakapo jiajiri mtaepukana na vitendo vya wizi, ubakaji na ujambazi,’’ alishauri katibu.
Aidha alieleza kuwa sera ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya uchumi wa buluu unaelekeza zaidi kwenye bahari, hivvyo aliwasisitiza viajana hao kukiendeleza kikundi chao kwa juhudi zote, jambo ambalo litawawezesha kupata ursa mbali mbali za kimaendeleo.
Mapema mwanakikundi Khadija Ali Juma alieleza kuwa ameamua kujiunga kwenye kikundi cha ujasiriamali, ili aweze kujipatia kipato kitakacho msaidia katika familia yake.
Aidha alisema mafanikio hayaji tu kama ndoto, hivyo ni vyema kuwa wavumilivu kupitia changamoto zinazowatokezea ili waweze kukiikisha mbele kikundi chao.
Akieleza changamoto zinazowakwaza kikundini hapo amesema ni vitendea kazi, ikiwemo mabero pamoja mapauro.
Mwenyye kiti wa kikundi hicho Khalfan Hamad Khalfan alieleza kuwa matarajio yao ni kuhakikisha wamekuwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya baharini.
‘’Tunatarajia kuzalisha Tani moja ya kaa, na Tani moja ya Kamba kila baada ya miezi miwili, na tani moja ya Samaki ndani ya kipindi cha mwaka mmoja,’’ alisema mwenyekiti.
Hivyo aliomba wizara ya uchumi wa buluu kujitokeza na kuwaunga mkono vikundi ambavyo vimewekeza juhudi zao kwenye maeneo ya bahari, ili waweze kunufaika na fursa zilizomo, ndani ya sera ya uchumi wa bluu.
Nae Afisa kutoka wizaa ya uchumi wa buluu Pemba Mohd Ali pamoja na wajumbe kutoka shirika la International Union for conservation of Nature [IUCN] walifika katika kikundi hicho na kuangalia maendeleo yao, na kuelewa changamoto zinazo wakabili wanakikundi hao na kuweza kutatuliwa.
Kkikundi hicho ambacho kinawanachama 17 wanaume 8, na wanawake 9, kilianzishwa rasmi mwaka 2013.