Friday, October 18

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  amehudhuria Maziko ya Mzee Said Kombo wa Kinazini – Wingwi

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Jumatatu Septemba 18, 2023 amehudhuria, pamoja na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Maziko ya Mzee Said Kombo wa Kinazini – Wingwi, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba

Mzee Said aliyefariki Dunia mapema jana Septemba 17, Hospitali ya Micheweni, amesaliwa katika Msikiti wa hapo hapo Kinazini na kuzikwa katika Makaburi ya Kijijini hapo.

Viongozi mbali mbali wa Serikali, Dini na Siasa wamehudhuria katika Maziko hayo wakiongozwa na Mratib wa ACT-Wazalendo Pemba, Bw. Said Ali Mbarouk.

Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amiin!

Innalillahi Waina Ilayhi Raajiun!

Kitengo cha Habari,
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,