Sunday, November 24

Virusi vya corona: Maswali 4 ambayo hayajajibiwa kuhusu chanjo ya corona

Maelezo ya picha, Maswali mbali mbali ambayo yanawatia hofu wanasayansi, serikali na raia yamesalia kutokuwa na majibu kuhusu chanjo

Kukimbizana na muda.

Hivi ndivyo tunavyoweza kuelezea uhamasishaji wa chanjo kwa wakazi wa dunia dhidi ya virusi vya corona na kurejesha hali ya kawaida kwa haraka iwezekanavyo.

Hadi kufikia tarehe 23 Januari, zaidi ya watu milioni 60 walikuwa tayari wamepata baadhi ya dozi za chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Lakini kadri nchi zaidi zinavyoanza au kuharakisha kampeni, mambo kadhaa yanasalia kutofahamika .

Bado haijawekwa wazi ni muda gani kinga ya chanjo inadumu baada ya kutolewa au kama aina mpya ya virusi ambayo imejitokeza kote duniani itakuwa sugu na kuifanya chanjo kutokuwa na ufanisi.

Takriban miezi miwili baada ya mpango mkubwa wa utoaji wa chanjo ya watu wengi kwa mkupuo ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia, tunaangazia maswali yanayosalia kuhusu chanjo za Covid-19.

1. Ni muda gani chanjo inatoa kinga ?

Jinsi gani mtu anaweza kuwa na kinga baada ya kupata chanjo ya virusi vya corona, swali hili ni mojawapo ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa sana katika miezi ya hivi karibuni.

Mwaka mmoja baada ya kuanza kwa janga, tafiti za kwanza kuhusu kinga ya muda mrefu tayari zimetolewa.

A patient after receiving a coronavirus vaccine in Poland
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Haijulikani ni kwa muda gani chanjo ya Covid-19 inaukinga mwili

 

Tafiti katika eneo hili ni hazina ufafanuzi mkubwa kuhusu hili na hii ni kutokana na ukweli kwamba hazijafanywa kwa muda mrefu kwasababu ya muda zilizochukua kutengeneza chanjo.

Lakini kwa mujibu wa taasisi ya masuala ya kinga ya mwili ya California – Taasisi ya La Jolla iliyopo California, baadhi ya watu waliopewa kinga wameweza kuonesha kuwa inaweza kuendelea kufanya kazi kwa takribani miezi sita.

Haya ni sawa na matokeo ya utafiti wa taasisi ya Afya ya umma ya England- Public Health England, ambao wanashauri kwamba wagonjwa wengi ambao walikuwa na Covid wana ulinzi wa kinga wa takribani miezi mitano.

Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kinga itadumu kwa muda mrefu, hata miaka.

Bila shaka, hili halitakuwa sawa kwa wagonjwa wote. Kila mmoja anaweza kuwa na ulinzi tofauti wengine kuwa na ulinzi zaidi au wa kiwango cha chini na uwezekano wa kuambukizwa tena utategemea hilo.

Kitu fulani kinachofanana hutokea kwa chanjo zote.

“Ni vigumu kusema ni kwa muda gani kinga ya mwili itadumu kwasababu ndio kwanza tumeanza kuwachanja watu na itategemea na mgonjwa na aina ya chanjo, lakini labda kati ya miezi sita na 12 ,” Dkt Julian Tang, mtaalamu wa virusi katika Chuo kikuu cha Leicester, nchini Uingereza ameiambia BBC.

A patient receiving a vaccine in the UK
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Kinga huwa na ufanisi baada ya chanjo itategemea aina ya chanjo na kama itamkubali mgongwa

Dkt Andrew Badley, profesa wa tiba katika kliniki nchini Marekani, ana matumaini : “Ninaamini kwamba athari za chanjo na kinga zinaweza kudumu kwa miaka kadhaa.

“Pia itakuwa muhimu kutathmini kwa kina visa vya watu walioambukizwa aina mpya za virusi na kuchunguza hai za wagonjwa baada ya chanjo.”

2. Je inawezekana kupatwa na corona baada ya kuchanjwa?

Ndio, inawezekana , na kwasababu mbalimbali.

Sababu ya kwanza ni kwamba kinga inayotolewa na chanjo nyingi haiiondoi hadi baada ya wiki mbili au tatu baada ya kupokea chanjo ya kwanza au dozi pekee, kulingana na aina ya chanjo.

“Kama utapatwa na virusi siku moja au wiki moja baada ya kudungwa sindano ya chanjo, bado kuna uwezekano wa kuambukizwa na unaweza kuambukiza watu wengine virusi ,” Dkt Tang anaeleza.

Two people social distancing in London
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Dkt Andrew Badley anasema baadhi ya data zinaonesha kuwa baadhi ya watu wanaweza kuendelea kuambukizwa Covid

Lakini hata kama mtu alipata virusi wiki kadhaa baada ya kupokea dozi inayopatikana, anaweza kuambukizwa.

” Data zilizopo zinaonesha kuwa baadhi ya watu wanaweza kuendelea kuwa na maambukizi Covid, japo wanaweza kuwa na virusi vichache na kutougua sana kuliko wale ambao hawajaambukizwa au kuchanjwa ,” Dkt Badley anaeleza.

” Kwa njia hiyo, ninadhani, kwamba virusi, wakati mtu fulani amechanjwa, itakuwa ni vigumu kusambaza virusi kwa mtu mwingine .”

Kwahiyo, kuna muafaka kwamba chanjo inaonekana kukinga idadi kubwa ya watu binafsi kwa ufanisi, lakini ni kwa kiwango gani inaweza kuzuia maambukizi na kusambaa bado ni jambo lisilojulikana.

3. Je chanjo itazuia kugeuka kwa umbo jipya la kirusi na aina nyingine za virusi za corona?

Hii inatia hofu.

Virusi hivi vimekuwa vikigeuka umbo na wakati mwingine hufanya hivyo kwa kiasi kwamba vinakua sugu kwa chanjo, kwahiyo vinahitaji kufanyiwa mabadiliko.

Aina ya virusi vya corona iliyobainika Afrika Kusini na Uingereza tayari imesambaa katika nchi nyingine na imesambaa kwa viwango vya hali ya juu.

A morgue in a South African hospital
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Virusi vya corona vimetengeneza aina mbalimbali za corona na kwa sababu hii kuna hofu kwamba itakua sugu

Moderna ilitangaza kwamba Jumatatu kwamba chanjo yake ilikua bado ina ufanisi dhidi ya aina za virusi vya Uingereza na Afrika Kusini, ingawa itatengeneza chanjo nyingine ya chanjo ya ziada ambayo inaweza kuboresha kinga.

Pfizer/BioNTech pia inadai kuwa chanjo yake inafanya kazi dhidi ya aina mpya za virusi vya corona.

“Sawia na hilo, inafaa kufahamika kuwa ingawa chanjo zilizoidhinishwa zina ufanisi sana, hazina uhakika wa ufanisi wa 100% dhidi ya aina mpya ya virusi vya corona, wala hata ile halisi ,” anasema Dkt Badley.

“Kina ya chanjo itategemea juu ya jinsi aina mpya za corona zilivyo ikilinganishwa na zile za awali ,” Dkt Tang aliongeza.

Kwa mukhtasari, serikali na idara za afya zitahitaji kufuatilia na kubaini aina mpya za corona zilizojitokeza ili kupata kuelewa iwapo dozi zilizopo zina ufanisi juu yake.

Amsterdam airport in the Netherlands
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Dharura ya aina mpya za virusi vya corona imesababisha kuwekwa kwa masharti ya kusafiri katika nchi nyingi

4. Kuna dozi ngapi na kwa kipindi cha muda gani chanjo inapaswa kutolewa ?

Chanjo za Pfizer, Moderna na ile ya Chuo cha Oxford/AstraZeneca , kwa mfano, hutolewa katika dozi mbili.

Mwanzoni, kwa kuzingatia ni dozi ngapi zilipimwa katika majaribio , watu waliambiwa kuwa watapata dozi ya pili baada ya wiki tatu hadi nne baada ya kupewa ya kwanza.

Lakini mwishoni mwa mwaka 2020, Uingereza ilitangaza kuwa itatoa kipaumbele cha kuwachanja watu wengi iwezekanavyo dozi ya kwanza na kwamba itatoa ya pili hadi miezi mitatu baada ya kupewa chanjo ya kwanza.

Iiibua mjadala wa kiamataifa juu ya njia bora ya kuchanja, lakini Pfizerna wengi katika jamii ya wanasayansi wengine duniani wangependa kuzingatia kile ambacho kimeidhinishwa katika majaribio ya maabara: dozi ya kwanza, halafu ya pili baada ya siku 21.

Shirika la afya duniani limetoa mwongozo kuhusu hii na pia lilipendekeza itolewe kila baada ya siku 21 au 28 28, ingawa walikiri kuwa kipindi hiki kinaweza kurefushwa hadi wiki sita katika visa visivyo vya kawaida.