Naibu Katibu, Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba ametembelea maeneo ya Malikale ya Mbuamaji na Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam na kuitaka Makumbusho ya Taifa la Tanzania kufanya utafiti zaidi juu ya malikale zote zinazopatikana katika maeneo hayo.
Kamishna Wakulyamba ametoa agizo hilo leo alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Makumbusho ya Taifa.
Amesema ni muhimu utafiti wa kina ufanyike ili kuweza kupata taarifa sahihi za malikale hizo, ambazo zitasaidia katika kuandaa ufasili wa malikale hizo.
” Fanyeni utafiti na kuweka maelezo ili anayetembelea aweze kuelewa” Amesema Kamishna Wakulyamba.
Naibu Katibu Mkuu ametembelea kituo cha taarifa na kumbukumbu Mbuamaji, msikiti wa kale wa karne ya 18, makaburi, visima vya kale na maeneo ya matambiko.