NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
AFISA mdhamini Ofisi ya Rais Ikulu Shuwekha Abdalla Omar, ameutaka uongozi na wafanyakazi wa bank ya NMB Kisiwani hapa, kuyafanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wateja wao ili kuimarisha utoaji wa huduma.
Alisema amaoni hayo nimuhimu kwa maendeleo ya bank hiyo, hivyo wateja wanapaswa kutoka maoni yao pale wanapoona kuna changamoto za utoaji wa huduma kupitia katika visanduku vya maoni.
Wito huo aliutoa wakati alipokua akizungumza na wateja na wafanyakazi wa bank hiyo, wakati wa uzinduzi ya wiki ya huduma kwa wateja duniani, ambayo huadhimishwa wiki ya kwanza ya mwezi wa Oktoba kila mwaka.
Alisema NMB inajitahidi kwa kiasi kikubwa katika matumizi ya kimtandao, wakati dunia imezidi kubadilika na bank hiyo imetoka na mobail, NMB mkononi sasa imekuja na huduma nyengine ambayo ni bora zaidi na mtu anaweza kufanya miamala ya fedha popote alipo.
“Mwananchi ambaye yuko kijijini na anataka kumpelekea mtu fedha sehemu yoyote, ambapo hawezi kufika mijini anatumia sasa hivi anatumia simu yake kwa kutuma fedha zake na mahitaji mengine pia anapata,”alisema.
Aidha mdhamini huyo aliutaka uongozi wa bank hiyo kuendelea kutoa taarifa juu ya huduma mbali mbali zinazotolewa na NMB, ikiwemo mikopo ya elimu ya juu, ili wanafunzi waweze kuomba na kuendelea na masomo yao.
Hata hivyo aliwataka wateja wanaotumia bank hiyo, kuzitumia fursa mbali mbali zinazotolewa, ili kuweza kuendelea vizuri wanahitaji maendeleo na zilipo fursa wanapaswa kuzitumia fursa hizo.
Mapema meneja wa NMB Pemba Hamad Mussa Msafiri, aliwashukuru wafanyakazi wa bank hiyo kuendela kutoa huduma bora kwa wateja wao, kwani huduma hizo ndio chachu ya wateja wengi kuendelea kuiamini bank hiyo.
Alisema wateja wao ndio wanufaika wakubwa wa huduma hali iliyowafanya kujumuika kwa pamoja na kufurahia wiki muhimu kwao kama bank na wateja kwa ujumla.
Nae meneja wa huduma kwa wateja kutoka bank ya NMB Wahbi Ahmad Alawi, aliwashukuru wateja wao kwa kuendelea kuwaamini katika kuweka amana zao, hali iliyoifanya NMB kua bank ya kwanza Tanzania na kushika nafasi ya Tatu kwa Africa.
Alisema NMB kwa Pemba inawateja zaidi ya elfu 40, hali inayoendelea kuifanya benk hiyo kuendelea kuaminiwa na wananchi, huku akiwataka wananchi kuendelea kuithamini na kuamini NMB.
Wakitoa maoni hayo baadhi ya wateja wameitaka bank hiyo kuendelea kutoa elimu kwa mawakala wao, ili kuwa waaminifu katika suala zima la fedha.
Mmoja ya wateja Omar Ali Salim, aliutaka uongozi wa NMB Pemba kuandaa bonanza maalumu, ili kuweza kujitangaza na kutangaza huduma zao pamoja na kuendelea kuwasajili wateja wapya.
“Kuna hili la vitundu vya kupokelea pesa au kuwekea pesa, hapa lazima mwende na wakati kuna kipindi watu kidogo tunaweza kupunguza ila kipindi cha watu wengi tuhakikishe pia tunaongeza watoa huduma,”alisema.
Nae Ibrahim Kambi Nyaka aliutaka uongozi wa NMB kuongeza ATM katika maeneo mengine, kwani kisiwa cha Pemba kina wilaya nne na wilaya ya Chake Chake tu ndio kwenye huduma hizo.
Hata hivyo aliishauri benk hiyo kuhakikisha wanafuatilia na kuyafanyia kazi malalamiko yanayotolewa na wateja wao, ili kuongeza ufanisi wa utoji wa huduma.
Kauli mbiu ya wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu, “Timu moja na Wewe”
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MWISHO