Thursday, February 27

RC Salama wataka wananchi kuitunza bahari

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, amewasihi wananchi kuendelea kuitunza bahari, kwani bahari ikiwa salama itapelekea kukuza uchumi wa bahari, ikizingatiwa dhamira kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutumia bahari katika uchumi.

Alisema mazingira bahari kuendelea kubakia salama ni jambo la muhimu, kwani kuna viumbe bahari na vinahitaji bahari na sisi wenyewe tunahitaji bahari, hivyo wadau na wananchi wanakila sababu kuhakikisha wanaendelea kuelimisha jamii.

Mkuu huyo wa Mkoa aliyaleza hayo katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi Zamani Wete, wakati akizungumza na wadau wa bahari hivi karibuni.

Aidha alisema ni muhimu kwa kila mmoja kusimamia mazingira ya usalama wa bahari, kwani mikakati mbali mbali inaendelea kufanywa ili kuona sera ya uchumi wa buluu inatekelezaka kwa vitendo.

“Kila mmoja wetu anawajibu wa kuhakikisha usafiri wa baharini utakuwa na mazingira salama, kila mmoja anaweza kutimiza utekelezaji wake,”alisema.

Alisema SMT na SMZ kupitia Wizara zake zenye dhamana ya usafiri wa bahari, zinaendelea kuchukua juhudi mbali mbali na kuhakikisha kuwa eneo la bahari lina kua salama muda wote, kutokana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na vyombo vya baharini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete Dr.Hamad Omar Bakar, alisema bahari ni muhimu kwa maisha ya wananchi, kwani hewa inayovutwa asilimia 50 inatoka baharini, ikizingatiwa bahari inamchango mkubwa kwa taifa.

Kwa upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Ibrahim Saleh Juma, alisema mategemeo makubwa ya warsha hiyo ni kuwafanya wananchi kufahamu umuhimu wa bahari kuwa salama.

Mapema Mwenyekiti wa bodi ya chuo cha bahari Dar es Salaam Kepten Ernest Bupamba, aliwataka vijana wa kike kutumia fursa ya kusoma masuala ya bahari, kwani fani hiyo sasa imekua na soko kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Alisema katika fani ya bahari wanawake wamekuwa na mwamko mdogo sana tafuati na wanaume, hivyo DMI inaendelea kuwahamasisha kutumia fura za kuinga na vyuo mbali mbali vya bahari, ili kupata makepteni wa meli wanawake kama ilivyo katika sekta ya anga.

Alisema sekta ya bahari imekusanya vitu vingi ikiwemo kilimo cha mwani, uvuvi, hivyo aliwataka watumiaji ya sekta hilo kuendelea kuhifadhi mazingira ya bahari kwani bahari imekua ni mkombozi mkubwa kwa wananchi.

MWISHO


Warning: file_get_contents(): http:// wrapper is disabled in the server configuration by allow_url_fopen=0 in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48

Warning: file_get_contents(http://api.xtrsyz.org/xt-visitor-counter/default.php?domain=www.pembapress.club&time=1740695377): Failed to open stream: no suitable wrapper could be found in /data/40/5/71/99/5397425/user/6768456/htdocs/portal/wp-content/plugins/xt-visitor-counter/xt-visitor-counter.php on line 48