Wednesday, January 15

Bodi yawataka wazazi kuendelea kuwasimamia watoto

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.

KATIBU wa bodi ya Taifa ya ushauri ya watoto Zanzibar (NCAB) Amne Mbarouk Ali, amewataka wazazi nchini kendelea kuwa wasimazi wazuri kwa watoto wao, kuwalinda dhidi ya mtukio maovu yanayoepeleka kutakitisha ndoto za watoto nchini.

Alisema moja ya ndoto za watoto waliowengi ni kupatiwa elimu bora, afya bora, malezi bora ambapo yote yamelezwa ndani ya  mikataba mbali mbali ya haki na ustawi wa mtoto.

 

Katibu huyo aliyaekeza hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, wakati wa mafunzo ya watoto juu ya kujua haki zao, yaliotolewa na jukwaaa la haki za watoto Zanzibar (ZCRF) kupitia mradi wa ZCRF imara na mtoto.

 

Aidha aliwataka watoto wenzake, kuachana na tamaa zinazoweza kupelekea kukiinguza katika vishawishi, ambayo mwisho wake vitawaingiza katika makundi maovu.

 

“Mafunzo haya tuliopatiwa yataweza kutusaidia kujua haki zetu, kutoa ushauri kwa jamii juu ya haki za mtoto, kujiamini na kupaza sauti zao dhidi ya matendo maovu yanayotokea,”alisema.

 

Nae mjumbe wa baraza la Watoto Wilaya ya Chake Chake Khamis Abdalla Mbarouk, alisema tokea kupata elimu tayari ameshavifikia vijiwe mbali mbali za vijana, kutoa elimu juu ya athari za uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya vitu ambavyo vinaweza kuwaingia katika matendo maovu.

 

Mapema Mwenyekiti wa Jukwaa la haki za watoto Zanzibar (ZCRF) Mussa Kombo Mussa, alisema suala la mmomonyoko wa maadili ni la mtambuka, lazima wazazi wajipange vizuri katika kulitokemeza ili kulinda maisha ya watoto wao.

Aidha aliwataka watoto wa kike kuwa mstari wambele, kukema vitendo viovu vinavyowakumbwa kwa kuhakikisha wanapaza sauti zao, ili wanaowafanyia vitendo hivyo kutiwa hatiani.

Akizungumzia lengo la mafunzo hayo, alisema ni kuwajenga vijana wa NCAB na mabaraza ya shehia, kuweza kujiamini kuzungumza pale wanapotakia kuzungumza, kwa kutoa ushahidi unaokubalika kwenye masuala ya udhalilishaji na kinachofanyika kwenye shehia zao.

“lengo letu ni kuwafanya vijana hawa kuweza kujiamini na kutoa taarifa za uhakika kwa kufuata takwimu sahihi, mwisho wa siku tuweze kutoa viongozi bora wanaojiamini kutoka katika mabaraza ya watoto, “alisema.

Nae meneja wa Mradi wa ZCRF imara na mtoto Sophia Leghela alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea watoto uwezo wa kufanya uchechemuzi na utetezi wa haki zao katika jamii.

Alisema wamelazimika kuwashirikisha watoto hao, kwa sababu wanataka kuona watoto wenyewe wanakua msatari wa mbele kwenye kudai haki zao.

MWISHO