Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imezidi kuimarisha mipango yake ya udhibiti wa ongezeko na kupunguza athari zinazosababisha uwepo wa maradhi ya saratani Nchini ikilenga kulipa umuhimu mkubwa suala zima la Afya bora kwa Wananchi wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo Afisini kwake Vuga wakati akianzisha Rasmi hamasa na vugu vugu kuelekea ndani ya Wiki ya maadhimisho ya Siku ya Saratani Ulimwenguni inayofikia kilele chake ifikapo Tarehe Nne Febuari ya kila Mwaka.
Mheshimiwa Hemed Suleiman amewataka Wananachi, na Wataalamu ambao tayari wameshakuwa na uzoefu na mazoezi kama hayo wakaendelea kushajiisha wananchi kushiriki kwenye upimaji wa maradhi hayo linalotarajiwa kufanyika Hospitali ya Wete Pemba kuanzia asubuhi ya Tarehe Pili Febuari Mwaka huu.
Mapema Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dr. Fadhil Mohamed Abdulla alisema mazoezi kama hayo ni muendelezo wa muda mrefu wa utoaji wa mafunzo ya jinsi ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza hapa Nchini.
Imetolewa na kitengo cha ahabari (OMPR)