NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
TAASISI ya Ifraj Zanzibar Foundation imekabidhi boti tatu za uvuvi, kwa vijana wa Shehia za Mvumuni, Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake na Mchakwe Wilaya Mkoani, ili ziweze kuwasaidia katika shughuli zao za uvuvi na kujiongezea kipato chao.
Akikabidhi boti hizo Mkurugenzi wa taasisi hiyo Pemba Abdalla Said Abdalla, alisema lengo kuu la Taasisi hiyo ni kusaidia vijana hao na kuwarahisishia kazi zao za uvuvi, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali ya Zanzibar katika dhana yake ya uchumi wa Buluu.
Hayo aliayeleza kwa nyakati tafauti wakati wa hafla ya kukabidhi boti hizo, pamoja na mashine zake kwa vijana hao ili kujishuhulisha na shuhuli zao za uvuvi.
Alisema sekta ya uvuvi ni moja ya sekta muhimu na inayomtoa kijana kwa haraka kuliko kazi nyengine, ndio maana serikali ya awamu ya nane imekuja na sera ya uchini wa buluu.
“Boti hizi kama mutazitumia ipasavyo, basi mafanikio makubwa mutayapata na mutaondokana na dhana na kusubiri ajira kutoka serikalini,”alisema.
Aidha aliwataka vijana hao kuvitumia vyombo hivyo katika matumizi salama, na kuepuka kuvitumia kwenye masuala ya magendo yakiwemo ya karafuu, mafuta, uvuvi haramuna na njia nyengine zozote ambazo serikali imekataza.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo aliwataka wananchi kuzitumia boti hizo, kwa ajili ya shughuli zao za uvuvi na wasiingize malumbano kupitvyombo hivyo, bali iwe ni chachu ya kujiongezea kipato chao na sio kuziweka rehani.
Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Mvumoni Khamis Ali Khamis, aliushukuru uongozi wa taasisi ya Ifraji Zanzibar Foundation, kwa kuwaona vijana wa shehia hiyo na kuwapatia vifaa hivyo vya uvuvi.
“Mimi kama kiongozi wa shehia hii nitahakikisha na kukisimamia ipasavyo chombo hichi na kinatumika kwa lengo lililokusudiwa la uvuvi,”alisema.
Nae Sheha wa Mfikiwa Bimkubwa Rajab Tangwi, aliishukuru taasisi ya Ifraji kwa kuwawezesha vijana kwenye shehia yake, sambamba na kuwataka wananchi hao kuitumia fursa waliyoipata kuwa mfano kwa vijana wenzao, kwani kukabidhiwa boti na mashine yake kutaondosha tatizo walilokuwa nalo la ukosefu wa ajira.
Nao vijana waliokabidhiwa vyombo hivyo waliishukuru taasisi ya Ifraji, kuahidi kuwa watavitumia vyombo walivyokabidhiwa kwa ajili ya uvuvi na kujiingizia kipato chao.
Mapema meneja wa Forodha Mkoa wa kikodi Pemba Suleiman Abdalla Said, aliyefika kushuhudia makabidhiano hayo amepongeza hatua ya Irfaji Zanzibar Foundation, kuwawezesha vijana na kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Boti hizo tatu za kisasa za uvuvi, zikiwa na mashine zake kila moja na makoti ya kuokolea maisha zimegharimu zaidi ya shilingi milioni 47,520,000/=.
MWISHO