NA AMINA AHMED-PEMBA.
WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba wameaswa kupaza sauti zao, katika kusaidia upatikanaji wa haki mbali mbali wanazoendelea kuzikosa watoto wanaofanyiwa udhalilishaji wa kijinsia kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo, kukosekana kwa sheria maalumu inayosimamia masuala ya udhalilishaji pamoja na ushahidi madhubuti na kupelekea kufutwa kwa kesi mbali mbali mahakamani kwa kuandika habari na makala mbali mbali.
Ameyasema hayo Mratibu wa chama cha Waandishi wa Habari TAMWA-Zanzibar kisiwani Pemba Fat-hiya Mussa Said alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa ofisi hizo Mkanjuni Chake chake katika mafunzo maalum kwa Waandishi juu ya kuandika changamoto zinazowakabili watoto walioathirika na vitendo vya udhalilishaji .
“Bado watoto waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia wanaendelea kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kukosa ushauri nasaha,kukosa fidia zao na kufutwa kwa kesi mbali mbali kutokana na kukosa ushahidi madhubuti watetezi wa kuzisemea changamoto hizi waandishi mnayo nafasi kubwa katika kuwasaidia kuzipatia ufumbuzi. “
Akitoa elimu juu ya sheria mbali mbali Siti Habibu Muhammed amesema serikali ya Zanzibar imeanzisha sheria mbali mbali mikataba ya kimataifa pamoja na mikataba ya kikanda katika kulipatia ufumbuzi suala la udhalilishaji hivyo ni vyema waandishi hao kuzitumia katika kuasemea mapungufu yanayopelekea kuongeza changamoto na vitendo vya udhalilishaji kwa waathirika hao.
Nao baadhi ya waandishi wa habari hao akiwemo Khadija Kombo wamesema wataendelea kuzisemea changamoto hizo kwa kuandika habari na makaa mbali mbali zitakazosaidia kuondoa changamoto hizo zinazoendelea kujitokeza kwa waathirika wa udhalilishaji.
Mafunzo hayo maalum yaluoandaliwa na Tamwa kwa Ufadhili wa Faundation for civil Society yamewashirikisha waandishi wa vyombo mbali mbali ikiwemo Radio, Tv, Magazeti pamoja na mitandao ya kijamii
Mwisho