NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
MWENYEKITI wa Kamati ya Ujenzi ya Skuli ya Michenzani Hamud Malim Khami, ameushukuru uongozi wa TRA Mkoa wa kikodi Pemba, kwa kuwakabidhi bati 50 zenye thamani ya shilingi Milioni 1,740,000/ ikiwa ni utekelezaji wa ahadi kwa skuli hiyo.
Alisema kwa sasa wanahitaji bati zisizopungua 300, kwa ajili ya uwezekaji wa bweni la wanafunzi wakike, wakati watakapokua wanakabiliwa na mitihani yao ya taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa bati hizo, kutoka kwa watendaji wa TRA Mkoa wa kikodi Pemba, huko Chokocho Wilaya ya Mkoani, ikiwa ni Wiki ya Shukurani kwa mlipakodi Pemba, ilioambatana na kauli mbiu “Kodi Yetu, Maendeleo Yetu, Tuwajibike” yalyoandaliwa na TRA Pemba.
Alisema kwa sasa bweni hilo linakabiliwa na changamoto zaidi, ikiwemo Milango, bati 250, madirisha, finishing yote ya jengo hilo, kitu ambacho kinaendelea kuwaumiza kichwa.
“Nyinyi wenzetu wa TRA mumeweza kusikia kilio chetu, lakini bado tunahitaji zaidi msaada ili vijana wetu watakapokua tayari kufanya mitihani waweze kutumia bweni hili kwa kukaa kambi,”alisema.
Naye Kaimu meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa kikodi Pemba, Nuhu Mohamed Suleiman, aliwataka walimu na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa skuli ya Michenzani, kufahamu kuwa TRA inakusanya kodi zote za Muungano na sio kodi za SMZ.
Alisema kodi hizo za Muungano ambazo zinakusanywa na TRA zinatumiwa kwa mahitaji ya Zanzibar, sambamba na ZRA inakusanya kwa niaba ya SMZ ambapi hutumiwa kwa ajili ya miradi ya maendeloe.
“Watau wamekua na wasiawasi kuwa kuna mamlaka ya mapotoa Tanzania na Mamlaka ya mapatoa Zanzibar, ni kweli kwa vile zanzibar ni nchi, iko katika muungano lakini pia Zanzibar itakua na vitu vyake wenyewe, katika suala la kodi,”alisema.
Hata hivyo alisema TRA inakusanya kodi za Muungano tu na sio kodi mbili, huku akiwataka walimu, wajumbe wakamati ya ujenzi kukakikisha wanakua mabalozi kwa wenzao, katika kuelimisha jamii juu ya kodi inayokusanywaa na TRA pekee.
Akizungumzia dhamira ya wiki ya shukurani kwa mlipakodi, alisema TRA imeamua kurudisha kwa jamii kile ambacho wanachokikusanya
Aidha alisema viongozi wanajitahidi kuhimiza juu ya suala zima la ulipaji wakodi, hali inayopelekea watendaji kukusanya mapato hayo yanaenda serikalini kwa ajili ya shuhuli za maendeleo.
Bweni hilo la wanafunzi wakike hadi sasa limeshafikia kuezekwa tayari limeshangarimu Jumula ya shilingi Milioni 28, huku hadi kukamilika kwake na kuanza kutumika zinahitajika Milioni 150.
MWISHO