Monday, November 25

HABARI PICHA: mahafali ya kwanza chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Pemba.

NAIBU waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Bdulghulam Hussein, akimkabidhi cheti mwanafunzi Bora Nairaty Rashid Khamsi aliyepata alama ya kwanza katika masomo ya Astashahada ya awali ya Uchumi katika maendeleo, wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere Kamapasi ya Pemba
NAIBU waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Bdulghulam Hussein, akizungumza na walimu, wanafunzi na wananchi mbali mbali katika mahafali ya kwanza ya chuo cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere Kamapasi ya Pemba, huko katika eneo la chuo hicho Pujini Wilaya ya Chake Chake.
NAIBU waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Bdulghulam Hussein, akiwatunuku Astashahada ya awali ya Maendeleo ya Jamii wanafunzi 18, wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere Kamapasi ya Pemba, huko katika viwanja vya Pujini Wilaya ya Chake Chake.
NAIBU waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Bdulghulam Hussein, akiwaongoza wanafunzi na viongozi mbali mbali katika maandamano ya kitaaluma kuelekea uwanja wa mahafali, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud na kulia ni Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalim Nyerere Tanzania Profesa Shadrack Mwakalila.
BAADHI ya wahaitimu wa fani mbali mbali katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalim Nyerere Kampasi ya Pemba, wakiwa katika maandamano ya kitaaluma kuelekea uwanja wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho, yaliyofanyika viwanja vya chuo huko Pujini Wilaya Chake Chake.
WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Madungu Wilaya ya Chake Chake wakiimba wimbo maalumu wa mahafali ya kwanza katika chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere kampasi ya Pemba, huko katika viwanja vya chuo hicho Pujini Wilaya ya Chake Chake

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)