Sunday, January 5

UTPC yaandaa maonyesho ya aina yake kwa vilabu vyake.

NA MWANDISHI WETU -DODOMA.

Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC, kwa mara ya kwanza umeandaa maonyesho ya vilabu vya waandishi wa habari yenye dhamira ya kuwezesha vilabu hivyo kupata fursa ya kuonesha na kueleza shuhuli zao wanazozifanya pamoja na kubadilishana uzoefu.

Maonesho hayo yamefanyika katika mtaa wa Uzunguni mjini Dodoma kwenye ofisi za UTPC ambapo kila Klabu imepata fursa ya kuonesha kazi zao kwa uwazi zaidi na kueleza mipango yao ya baadae ya kuimarisha vilabu hivyo.
Wakitembelea katika mabanda mbali mbali ya maonesho hayo Wadau na Viongozi wa UTPC wakiongozwa na Rais wa muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania, Deogratius Nsokolo walipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Klabu hizo ambapo walionesha kuvutika na utendaji kazi wa Klabu hizo.
Baadhi ya Wadau waliotembelea banda la Klabu ya waandishi wa habari ya Pemba Press club wakiwemo wamiliki wa Fresh TV Tanzania online Mike Mambu aliipongeza Klabu hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuishauri kuanzisha miradi mikubwa ya kiuchumi ambayo itasaidia kuiendeleza klabu hiyo.
Amesema kwa kuwa zao la mwani linalimwa kwa wingi Pemba sio vibaya na PPC wakaamua kuanzisha shamba lao litakalowasaidia kuiendesha klabu hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa UTPC Kenneth Simbaya aliipongeza Klabu ya waandishi wa habari Pemba kwa kazi wanazozifanya na kuwahimiza kuwa shughuli zote wanazozifanya kuziandika katika maandishi maalum ili kuwa na kumbukumbu badala ya kuziweka
Alifahamisha kuwa mawazo hayo yakiandikiwa vizuri na kuratibiwa vyema yanaweza kuipatia fedha PPC kwa ajili ya maslahi ya klabu yao..
MWISHO.