Sunday, November 24

Kilio cha upatikanaji wa maji safi na salama bweni la skuli ya Madungu Sekondari chamaliza.

 


NA AMINA AHMED-PEMBA.
KWA zaidi ya Miezi mitatu na siku kadhaa sasa hofu ya usalama wa afya kwa baadhi ya wanafunzi wanaokaa katika bweni Skuli ya Madungu sekondari imeondoka hii ni baada ya kupatikana huduma ya maji safi na salama muda wote skulini hapo, sambamba na kuwepo kwa utaratibu maalum wa uzolewaji wa taka katia eneo wanalotumia kutupa taka mbali mbali.

Wakizungumza na habari hizi baadhi ya wanafunzi wanaokaa katika bweni skulini hapo wamesema  kuwa hali ya kuishi kwa wasi wasi na hofu ya maradhi kwa sasa imeondoka hali ambayo imesaidia kuzidisha umakini zaidi katika masomo yao.

Aidha wamemshukuru mwandishi wa habari hizi kwa jitihada aliyochukua katika kuhakikisha suala hili linakuwa sawa na kupatiwa ufumbuzi.

“Nilipoona maji yanatoka siku iyo hayajafungwa ata mara moja nikajiuliza kwaio waandishi wanaogopewa malalamiko yetu yanasikilizwa mara moja nilifurahi sana nilitamani ungerudi siku ile ile uone tulivyojaa furaha”. amesema mwanafunzi Faidhat Adam Kombo

 

Katika suala la usafi amesema wanaohusika na usafi kutoka serikalini wanapita kila baada ya siku mbili na kuondoa taka taka wakati hapo   awali zilikuwa zinarundikana wala haziondolewi haraka.

Hata hivyo wanafunzi hao wamewaomba wahisani wadau na serikali kuwasaidia tena upatikanaji wa matanki mengine ya kuhifadhia maji ili yarahisihe zaidi huduma hizo kwa wanafunzi hao.

” Matanki yapo ila kutokana na ukubwa na wingi wa wanafunzi halitoshi tunaomba wadau wengine wajitokeze kutusaidia matanki makubwa ili tuhifadhi maji”amesema mwanafunzi  Aisha Omar Abdalla

Awali wanafunzi wa kike skuli hiyo walionesha hofu juu ya usalama wa Afya zao kutokana na kukosekana kwa huduma ya uhakika ya maji safi na salama pamoja na kuwepo kwa mrundikano wa taka ambazo huchukua muda kuondolewa ambapo kwa sasa changamoto hizo zimeondoka.

MWISHO.