Wednesday, October 30

MATUKIO KATIKA PICHA, UFUNGUZI WA NYUMBA NNE ZA GOROFA ZA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA ABDALLA MZEE MKOANI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekieti wa baraza la Mapiduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, leo amefungua na kukabidhiwa rasmi Nyumba za Wafanyakazi wa Abdalla Mzee Hospitali Mkoani, ufunguzi huo umefanyika kwenye hospitali hiyo, viongozi mbali mbali wa Wizara ya Afya, wananchi wamehudhuria.

Serikali ya China imewakilishwa na balozi Mdogo wa China Zanzibar Zhang Ming

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati)kikata utepe kuashiria ufunguzi wa Nyumba za wafanyakazi wa Abdalla Mzee Mkoani, kulia ni Balozi Mdogo wa China Zanzibar Zhang Ming, kushoto kwa Rais ni Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, na viongozi mbali mbali wa serikali Unguja na Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akipokea ufunguo wa nyumba za wafanyakazi wa Abdalla Mzee Hospitali kutoka kwa balozi Mdogo wa China Zanzibar Zhang Ming, huku waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akishuhudia zoezi hilo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akipata maelezo kutoka kwa katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Habiba Hassan Omar, mara baada ya kukagua moja ya chumba cha wanyakazi wa Abdalla Mzee Hospitali Mkoani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bazara la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikagua moja ya majiko yaliyomo ndani ya nyumba za Wafanyakazi wa Abdalla Mzee Hospitali Mkoani, kushoto ni Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, mara baada ya kuzifungua rasmi nyumba hizo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, akiwa na viongozi mbali mbali wa serikali Zanzibar wakiwasili katika hafla ya ufunguzi wa Nyumba za Wafanyakazi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Hospitali Mkoani
BALOZI Mdogo wa China Zanzibar Zhang Ming akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Nyumba za Wafanyakazi wa Abdalla Mzee Hospitali, hafla iliyofanyika katika hospitali hiyo Mkoani
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt.Habiba Hassan Omar, akitoa taarifa ya Kitaalamu juu ya ujenzi wa Nyumba za Wafanyakazi wa Abdalla Mzee Hospitali Mkoani, hafla iliyofanyika Katika hospitali hiyo Mkoani
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, akitoa salamu za wananchi wa mikoa miwili ya Pemba, katika hafla ya ufunguzi wa Nyumba za wafanyakazi wa Abdalla Mzee Mkoani Hafla iliyofanyika katika hospitali hiyo.
WAZIRI wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa nyumba za wafanyakazi wa Abdalla Mzee Hospitali, hafla iliyofanyika katika hospitali hiyo Mkoani
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali mwinyi, akizungumza na Wananchi wa Mikao Miwili ya Pemba, wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Abdalla Mzee Hospitali Mkoani, hafla iliyofanyika katika hospitali hiyo