Thursday, December 26

TAMWA YAWAKA WAANDISHI KUPAZA SAUTI ZA WANAWAKE NA MABADILIKO TABANCHI

NA ABDI SULEIMAN.

WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba, wameshauriwa kujikita zaidi katika kuandika habari zitakazo saidia wanawake kupaza sauti zao, katika masuala ya mabadiliko ya Tabianchi na athari zake.

Hayo yameelezwa na Afisa mawasiliano kutoka TAMWA Zanzibar Nafda Hindi Mohamed, wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari, kupitia mradi wa Zanz Adapt mkutano uliofanyika Ofisi ndogo za TAMWA Mkanjuni Chake Chake Pemba.

Alisema iwapo sauti za wanawake zikisikika ipasavyo basi, zitasaidia kuondoa changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika maeneo mbali mbali na kusaidia kupata haki zao zinazokosekana kutokana na kutokusikika kwa sauti zao.

Afisa huyo alisema, wameamua kutoka mafunzo hayo kwa sababu, wamefanya utafiti na kugundua kwamba habari za wanawake na uongozi, bado zinaandikwa kwa kiasi kidogo katika masuala ya mabadiliko ya Tabianchi, wakati ndio waathirika wakubwa yanapotokea mafuriko na majanga mbali mbali.

“Sote ni mashahidi wanawake ndio waathirika wakubwa wa mabadiliko ya Tabianchi, sasa tunataka sauti zao zisikike kwa wingi katika masuala ya wanawake na uongozi,”alisema.

Hata hivyo aliwataka waandishi wa habari, kuzungumzia masuala hayo ili jamii kujuwa kinachowaathiri wanawake katika mabadiliko ya tabianchi.

Alisema mabadiliko ya tabianchi ni janga la kitaifa na wanawake ndio waathirika wakubwa kwenye mabadiliko hayo, kutokana na kutokuonekana kwa machangao wao na sauti zao kusikika, kesi nyingi zipo na waathirika wakubwa ni wanawake.

Kwa upande wake Mjumbe wa bodi kutoka chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar Mwatima Rashid Issa, alisema imeonakana kwamba mwanamke ananafasi kubwa katika masuala ya mabadiliko ya Tabianchi, kwani kuna changamoto za hali ya hewa zinavyotokezea.

Alisema kuna mazungumzo madogo, yanayowazungumzia wanawake katika masuala ya uongozi na mabadiliko ya Tabianchi, yanapotokea anaweza kukabiliana nayo.

“lengo ni kumuonesha manamke kuwa yuko juu, imeonekana kwamba mwanamke yuko chini katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi,”alisema.

Kwa upande wake Mwandishi wa habari kutoka Zanzibarleo Habiba Zarali Rukuni, alisema mabadiliko ya Tabinchini janga lililoikumbwa dunia, waanawake ndio waathirika wakubwa hivi ni wakati wa kuandika habari za mabadiliko hasa kwa wanawake ikiangaliwa ndio waathirika wakubwa.

Nae Mwandishi wa habari kutoka Radio Jamii Micheweni Time Khamis Mwinyi, alisema kufanyika mafunzo hayo kutawezesha wanawake sasa kusikika kwa sauti zao katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabinchi.

MWISHO