AFISA Mdhamini Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Pemba Abdulwahab Said Abubakar, amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo Pemba kufanyakazi zao kwa kushirikiana ili kuweza kufikia malengo ya serikali ya awamu ya nane katika kuwatumikia wananchi.
Alisema serikali ya awamu ya nane imehimiza mambo mengi, ikiwemo suala la uwajibikaji, utoaji wa huduma bora kwa wananchi, hivyo Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais ndio Wizara mama katika suala la utoaji wa huduma.
Mdhamini huyo aliyaeleza hayo mara baada ya kukabidhiwa Ofisi hiyo, kutoka kwa Afisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Pemba Ibrahim Saleh Juma, hafla iliyofanyika Gombani na kushuhudiwa na watendaji kutoka vitengo mbali mbali vilivyochini ya Wizara hiyoo.
Aidha alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekitiwa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa kumpatia nafasi hiyo huku akiahidi kuendeleza utamaduni mzima wa kutoa mashirikiano na kuyaendeleza mazuri yote yaliyopo.
Akizungumzia suala la uwajibikaji, mdhamini Abdulwahab aliwataka wakuu wavitendo na maidara kuwajibika ipasavyo na kuweka mbele uzalendo wa nchi wakati wakufanya kazi zao.
“kama kuna changamoto zozote tutazitatu kwa ufanisi mkubwa, ila tunapaswa kuongeza kasi ya kubuni mambo na kuweka vitu vipya katika taasisi zetu”alisema.
Hata hivyo alitawaka watoaji wa huduma kuhakikisha wanatumia lugha nzuri wakati wautoaji wa huduma zao, pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi wlaiowazunguka.
Mapema aliyekua afisa mdhamini wa Wizara hiyo ambaye pia ni Afisa Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba Ibrahim Saleh Juma, aliwataka wakuu wa vitengo ndani ya wizara hiyo kuhakikisha wanayaendeleza mazuri yote waliokua nayo, pamoja na kasi ya utendaji iliyopo kwa sasa.
Alisema ofisi ya Rais Fedha na Mipango ni Ofisi mama, kwani wizara zote Pemba zinategemea ofisi hiyo, alimtaka mdhamini mpya kuhakikisha anashirikiana na maafisa hao ili kuweza kufikia malengo ya wizara na kufanikiwa.
“Kua mstahamilivu na pia unapaswa ufuatilia kiti lazima kuna muda kiwe hakikaliki, kufuatilia utendaji wa kazi katika vitendo vyao hapo utaweza kufanikiwa”alisema.
Hata hivyo alimtaka kutambua kuwa serikali inatengemea sana wizara hiyo kupitia ZRB katika suala zima la ukusanyaji wa kodi, hivyo alimtaka kulitunza na kulithamini jengo zima hilo.
Akitoa neneo la shukuran kwa niaba ya taasisi zinazojitegemea Jamal Hassan Jamal, aliwashukuru maafisa wezake kuendelea kutoa mashirikiano kwa mdhamini mpya ili kufikia malengo.
Kwa upande wake Afisa Mipango na Bajeti Firdaud Khatib Haji, aliahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa kiongozi huyo mpya, ili kuweza kufikia malengo ya serikali.