Monday, November 25

MAMBO MATANO KUHUSU MAALIM SEIF

1. Amekuwa jabari la kisiasa na mmoja wa wanasiasa nguli barani Afrika na Duniani katika karne ya sasa.
2. Amekuwa Chuo Kikuu cha Kisiasa, yaani ‘He was a Political University by himself,’ ungeliweza kufanya tafiti nyingi kuhusu siasa zake na fikra zake na ukaandika maelfu ya vitabu na bado ukahitaji kuandika tena na tena.
3. ‘He was an institution by himself’ (alikuwa taasisi inayojitegemea). Alikuwa na uwezo wa kufanya siasa ziwe na mwelekeo fulani na zikatii na mkabaki mnashangaa amewezaje. Kwa sasa siasa za upinzani za Zanzibar hazina tena “mtu taasisi”…hakuna ambaye anaweza kuwa hivyo isipokuwa Seif ambaye sasa hayupo.
4. Alikuwa bingwa wa maridhiano na kutaka watu wakae pamoja. Kwenye hili unaweza kumpa digrii 10. Hata kama ungalimuudhi na kumuumiza Maalim kiasi gani, kesho asubuhi angalikupigia simu na kukusalimu na kukwambia bado anakuthamini. Alikuwa na roho ya ajabu sana.
5. Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kusikiliza. Kwenye vikao, ninyi mnaweza kuzungumza masaa 10 yeye anasikiliza na hawezi kuwaingilia, alikuwa anasikiliza sanaaaa. Wakati mnazungumza yeye huandika kila kitu, na haachi hata nukta, halafu yeye anaongea mwishoni kidogo. Muhtasari wake mfupi wa mwishoni ungeliwafanya mjue mwelekeo na mjue nani alibwabwaja na nani alizungumza mambo ya msingi.
Narudia, ‘A VERY BIG LOSS TO THE NATION’.
R.I.P Mzee.
Your Long Time Political Child,
Julius S. Mtatiro
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru