NA ABDI SULEIMAN.
WANANCHI wa Kisiwa cha kidogo cha Kokota Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba wameishukuru taasisi ya Milele Zanzibar Foundatio, kwa kuapatia boti ya kuvukia kisiwani huko.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya makabidhiano ya boti hiyo huko katika bandari ya Kivumoni Mtambwe Kusini, baina ya Uongozi wa Wilaya, wananchi wa Kokota na Taasisi ya Zanzibar Milele Foundation.
Wamesema kuwa boti hiyo itawasaidia sana katika harakati zao kisiwani huko, katika kufuata huduma mbali mbali eneo la wete au Mtambwe, ikiwemo kuwapeleka wanafunzi skuli, walimu na wagonjwa wanapohitaji huduma za dharura hospitali ya Wete.
Ali Omar Khamis alisema Taasisi ya Mililele imefanya jambo kubwa sana kwa wananchi wa Kokota, huku akiwataka wananchi wenzake kuhakikisha wanaitunza na kuithamini boto hiyo.
“Leo tumeanza kupiga hatua tena kimaendeleo, kwa muda mrefu tulikuwa tukipata usumbufu katika suala zima la kuvukia, sasa milele wametusaidia jambo zuri sana”alisema.
Mariyam Ali Othman alisema akinamama walikuwa wakipata tabu sana wakati wanapohitaji usfiri kwenda kufuata huduma mijini, hali inayowalazimu kuvuka, wakati mwengine kipindi cha upepo tabu inazidi sana.
“Kipindi cha upopo mkubwa kama saivi upepo wakusi, hata wanafunzi wanaohitaji kwenda skuli ngambu huwa usumbufu sana, wakati mwengine wanakatisha hata safari”alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahya, aliipongeza taasisi ya Milele Zanzibar Faoundation, kwa kuwapatia msaada wa boti kwa wananchi wa Kokota, usafiri ambao utawasaidi sana katika harakati zao za usafiri.
Aidha mkuu huyo aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanakitunza na kukithamini chombo hicho ili kiweza kudumu kwa uda mrefu, pamoja na kuwasaidia katika harakati za kuvuushana kisiwani huko.
Mkuu huyo wa wilaya aliweza kuwanasihi wananchi wa Kisiwa cha Kokota, kutokuingiza migogoro na migongano ndani ya boti hiyo, kwa wale watakaokabidhiwa, pamoja na kutokujimilikisha kufanya hivyo ni kinyume na maelekezo ya boti hiyo kutoka ka mfadhili.
“Tunapaswa kufuata taratibu za boi hii inavyotakiwa, isije ikatumiwa kwa kuvulia, pamoja na kusafirishia magendo kufanya hivyo ni kwenda kinyume na malengo ya boti hiyo”alisema.
Hata hivyo aliwataka wadau wengine kujitokeza kwa wingi kusaidia usafiri kwenye baadhi ya visiwa vilivyobakia, kwani wilaya ya wete imejaaliwa kuwa visiwa vidogo vidogo vingi.
Kwa upande wake mratib wa taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Abdalla Said Abdalla, alisema shehia ya Mtambwe Kusini ni miongoni mwa shehia ambazo zimo katika miradi yao, hivyo kutokana na kukosekana kwa usafiri wa uhakika wamelazimika kukabidhi boto hiyo.
alisema tayari kisiwa cha Kokota walishakipelekea huduma ya maji kupitia baharini, ambapo zaidi ya milioni 300 zilitumika, ambapo kwa sasa wanaendelea kupeleka maji katika kijiji cha Makongeni Mtambwe Kusini mradi uliogharimu Milini 39.
“hii boti inabeba abiria 20 wakiwemo watoto watano, boti hii isije ikatumiwa kwa shuhuli za maharusi, kuvulia na hata shuhuli nyengine ambazo haziendani na matakwa ya mfadhili, ikizingatiwa boti imegharimu fedha nyingi shilingi Milioni 39.8”alisema.
Akitoa neno la shukurani Mkurugenzi wa baraza la Mji Wete Salma Abuu Hamad, aliishukuru taasisi ya milele Zanzibar Faoundation kwa kuwapatia boti wananchi wa Kokota, huku akiiyomba milele kukitumia macho na kisiwa cha Njau kilichoko Gando.