Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema serikali ya mapinduzi Zanzibar inathamini mchango wa vyuo vikuu Nchini katika kuwafinyanga wataalamu wa fani mbali mbali wanaowezesha kuchangia maendeleo ya Taifa.
Rais Dk. Hussein Mwinyi ameleza hayo katika hotuba iliosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika mahafali ya 20 ya chuo cha Abdulrahman Al Sumait kilichopo Chukwani nje kidogo ya jiji la Zanzibar.
Mhe. Hemed ameleza kuwa, hivi sasa Zanzibar inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo wanafunzi wa darasa la 12 kutokufanya vizuri katika mitihani yao pamoja na kuwepo kwa changamoto ya matendo ya udhalilishaji aliviombo vyuo vikuu nchini kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto hizo.
Akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali ambae pia ni Kaimu waziri wa wizara ya Afya Mhe. Simai Mohamed Said amewaomba wahitimu kutorizika na elimu walioipata na badala yake wajiendeleze na hatua nyengine ili waweze kujijengea msingi imara wa kupambana katika soko la ajira.
Nae Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Msafiri Mshewa amesema chuo kimekuwa kikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kushuka kwa idadi ya udahili wa wanafunzi kulikosababishwa na mabadiliko ya sifa na vigezo viivyowekwa na tume ya vyuo vya elimu ya juu Tanzania (TCU) na mamlaka ya vyuo vya ufundi Tanzania (NACTE).
Katika mahafali hayo ya 20 ya chuo cha ABDULRAHMAN AL-SUMAIT jumla ya wahitimu Mia Mbili (200) wamehitimu mafunzo yao kwa ngazi ya Shahada, Stas-shahada na Astas-shada kupitia fani ya Sanaa na Syansi ya jamii.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Febuari 27,2021.