MENEJA kamopeni za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Aboud Mohamed amewataka wananchi wa jimbo la Ole Wilaya ya Chake Chake, kuitumia bahati ya kipekee ya kupata viongozi wenyenia ya kuwatumikia wananchi wajimbo hilo
Alisema jimbo la ole katika miaka mingi iliyopita, lilikuwa chini ya utawala wa chama cha CUF, huku wananchi wakikosa maendeleo waliokuwa wakiahidiwa na viongozi walioowachagua.
Meneja huyo aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akiwanadi wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani wa jimbo hilo, katika mkutano wa hadhara wa kampeni zilizofanyika unja wa mpira Vumba Vitongoji.
Alisema wananchi wa jimbo la Ole wanakila sababu kuwachagua wagombea wa wote wa CCM, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili viongozi hao waweze kuwatumikia.
“Kazi yenu ni kwenda kupiga kura tu, CCM imeshashinda tena saa nne za asubuhi ikiwa utapiga kura na ushindi wa mwaka huu inashinda kwa kishindo kwa asilimia 90%”alisema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Mohamed Ali Khalfan, aliwataka wananchi kutokufanya kosa Oktoba 28, kwani wananchi wanahitaji maendeleo.
“ikulu sio sokoni kama kila mtu anapaswa kwenda, ikulu ni sehemu muhimu na wanaoingia ni watu maalumu, wananchi ni wajibu kuunga mkono ccm”alisema.
Mjumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, alisema wananchi wa ole wanahitaji maendeleo na vijana ndio viongozi wanaotarajiwa kuongoza nchi.
Aidha aliwataka wananchi wa Ole baada ya kupiga kura kurudi majumbani na sio kubaki katika vituo, huku akiwataka wananchi kutokukubali kuingia barabarani.
Kwa upande wake aliyekuwa mbunge wa jimbo la chake chake kupitia CUF, ambae kwa sasa ni mwanachama wa CCM Yussuf Kaiza, amesema kuwa chama cha Mapinduzi ndio kimbilio la vijana kutokana na ndio chama chenye kuwajali vijana na ndio chenye sera bora.
Naye balozi mstaafu na mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Chake Chake, alisema bila ya wanaCCM kupiga kura na kukuchangua chama cho, basic cm haiwezi kushinda hivyo aliwaomba wananchi kuichagua CCM uchaguzi utakapokuja.
Nao wagombe ubunge na uwakilishi jimbo la Ole waliwataka wananchi kutokufanya kosa katika uchaguzi utakapofika, kwa kuhakikisha wanawachagua ili kuwaletea maendeleo.