NA ABDI SULEIMAN.
MWAKILISHI wa Kuteuliwa Viti maalumu kupitia wasomi Lela Mohamed Mussa, amewataka wanafunzi wa wanawake kuhakikisha wanaongeza nguvu katika masomo ya sayansi, ili kupata wataalamu watakaoweza kusaidia maendeleo ya nchi yao.
Alisema iwapo watasoma kwa bidii masomo ya sayansi wataweza kuibua wataalamu wazuri na watakaoweza kusaidia ndugu zao kuwapunguza gharama za kufuata matibabu nje ya Zanzibar.
Mwakilishi huyo wa kuteulia, aliyaeleza hayo huko katika skuli ya Madungu sekondari, mara baada ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya ujenzi wa dahalia la wanawake, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake Dunini.
Alifahamisha kuwa lengo la kukabidhi vifaa hivyo ni kuhakikisha jengo la dahalia linamalizika na wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri.
Aidha aliwataka wanawafunzi wenzake kupambana na kutokukata tama, katika masomo yao licha ya kukumbana na changamoto nyingi ambazo zinaweza kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Akizungumzia suala la udhalilishaji, Lela ambae pia ni Waziri wa Utalii na Mambo ya kale Zanzibar, aliwataka wanafunzi kupiga vita matendo ya unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsi, kwani yamekuwa yakiwanyima uhuru wanawake na watotio nchini.
Kwa upande wa suala la Chakula kwa skuli hiyo, aliwataka wanafunzi hao kujishuhulisha na masomo tu, kwani viongozi wao wapo na watashuhulikia tataizo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Mpendae Unguja Toufiq Turky, aliwasihi wanafunzi hao kuendana na ndoto zao katika kusoma kwao, kwani kusoma sio kupasi tu.
Alisema kutokana na mabadiliko ya matumizi ya mitandao dunini, itafika wakati sehemu ya watu watatu inafanya na mtu mmoja tu, huku akili ya binaadamu itakua haifanyi kazi tena.
“Leo kila mtu unaomuona nasimu kubwa hapa na tafuta kitu kilichopo marekani, vizuri kila mtu kufuata ndoto zake katika kusoma na kufikia mbali”alisema.
Katibu wa CCM Mkoa wa kusini Pemba Mohamed Ali Khalfan, alisema kazi ya viongozi waliopo madarani ni kusaidia huduma za kijamii, ikiwemo suala zima la skuli hiyo.
Alisema chama cha mapinduzi kimepata viongozi wazuri ambao wanasaidia moja kwa moja huduma za kijamii, tafauti na miaka iliyopita.
Naye mwalimu mkuu wa Skuli ya Madungu Sekondari Mohamed Shamte Omar, alisepongeza serikali ya awamu ya nane kwani I serikali ya vitendo zaidi, huku akiwataka wanafunzi kulipa msukumu suala la kusoma masomo ya sayansi zaidi.
Aidha Mwalimu huyo aliwataka viongozi hao wa majimbo kuhakikisha wanaongeza nguvu zao skulini hapo, ili kuona wanaufunzi wanasoma na kulala katika mazingira mazuru.
Mwakilishi wa kuteuliwa kupitia viti maalumu wasomi Lela Mohamed Mussa, kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Mpendae Toufik Turky, wamekabidhi mbao, taizi, saruji, nondo, Jipsam bord vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 750,000/=.