Monday, November 25

Wanawake watakiwa kujenga tabia ya kujiangalia kwa karibu mwenendo wa afya zao

Dr Ummukulthum Omar Hamad daktari bingwa wa magonjwa ya kike akitoa mafunzo juu ya Magonjwa ya akina mama kwa waandishi wa habari wanawake hiking Tunguu ikiwa ni siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa TAMWA.

NA KHADIJA KOMBO.

Wanawake  wametakiwa kujenga tabia ya kujiangalia kwa karibu mwenendo  wa afya zao ili waweze kujigundua mapema iwapo kuna dalili zozoe za Maradhi  wafatilie tiba kwa haraka
Wito huo umetolewa na Dr. Ummukulthum Omar Hamad  wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wanawake juu ya magonwa ya akina mama yakiwemo Cansa ya  shingo ya uzazi na Cansa ya matiti huko katika ukumbi  wa ofisi za TAMWA Zanzibar  Tunguu ikiwa ni kuelekea siku ya mkutano mkuu 2021.
Amesema kawaida ya maradhi yanaingia kidogo kidogo hivyo utakapo jigundua mapema unaweza kupata tiba kwa haraka.
Amesema hivi sasa kuna magonjwa mengi ambayo yameikumba Jamii hususan wanawake  kama  vile Sukari,  Cansa ya Shinji ya uzazi na Cansa  ya matiti lakini wanashindwa kujigundua  kutokuwa na utamaduni wa kukagua miili yao.
Amewashauri wanawake hasa waliofikia umri wa miaka 45 kuhakikisha wanafanya uchunguzi Mara kwa Mara kwani huo ni umri hatari ambao maradhi mengi huanza kujitokeza.