Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman Sharif amewataka Wazanzibar kuendeleza mshikamano uliopo ili juhudi za kukuza uchumi kwa haraka ziweze kufanikiwa kwa haraka.
Makamu huyo aliyaeleza hayo huko Msikiti wa Jibril Mjini Unguja mara baada ya kuswali swala ya Ijumaa akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashidi Msaraka.
Alisema hali ya maisha ni mbaya miongoni mwa Wazanzibar hivyo juhudi za pamoja ni muhimu wakati huu ambapo Zanzibar ina mfumo wa Serikalin ya Umoja wa Kitaifa.
“Tukiweka mbele mshikamano basi maisha yetu yatakuwa bora katika kipindi kifupi lakini tukibeza mshikamano tutaharibikiwa” alisema Masoud.
Alisema sichengine ambacho kitaito Zanzibar hapa ilipo isipokuwa ni kuendeleza mshikamo uliopo ambao ulitokana na maridhiona ya viongozi wakuu.
Alisema ni jambo la kufurahisha kuwa Zanzibar imepata Rais ambaye anapenda uwepo mshikamano na kueleza kuwa hakuna budi kumuunga mkono katika juhudi za kuleta maendeleo ili iwe Rais kwake kuwahudumia wananchi.
“Ni vyema viiongozi wakiwa wamoja basi na wale wanaongozwa kuwa wamoja , hapo tutafanikiwa kwa haraka” alisema Makamu huyo.
Alisema kama walivyo viongozi wema basi na wale wanaongozwa wanatakiwa kuwa katika hali hiyo na dhamira ya dhati.
Alisema Viongozi wanaaza kwenye familia na itakuwa vyema wazanzibar wakaazijenga familia zao kwa kile alichokieleza kuwa ndio mwanzo wa viongozi waadilifu.
“Sitochoka kukuombeni kila mmoja kwa namna yake apiganie kwa namna yake kuendeleza maridhiano kwa dhamira njema kwani hiyo ndio dua njema kwetu “ alisema Masoud.
Aidha aliwataka waumini hao walijumuika katika swala hiyo kuwaombea viongozi wao ili waweze kuiongoza nchi katika hali ya usawa na amani. Kwa upande mwengine aliwataka wauminin hao kutoacha kumkosoa pale wanapoona anakwenda kombo katika uongozi wake na kumuweka katika mstari ulionyooka.
Awali akitoa Khutba katika ya Swala ya Ijumaa Khatib Sheikh Saadat Iman Saadat aliwataka waumini kufata nyayo za Mtume Muhammad SAW na kuwa na subira na ustahamilimu huku wakiendelea kuomba dua za kuendeleza Maridhiano yaliopo na hasa miezi hii mitukufu ambapo kiongozi huyo wa Umma alikabidhiwa Swala.
Aidha alimnasihi Makamo huyo wa Kwanza wa Rais pamoja na viongozi wengine kutembelea mitaani na kuona hali za wananchi pamoja na mahospitali na barabarani na kuacha kungojea kuletewa ripoti na maafisa ambazo hazina uhalisia wala ukweli wowote.
“Kiukweli Maisha ya watu ni magumu na itakuwa vyema viongozi mkashuka chini zaidi watu ili mujionee maisha yanavyowawaumiza wananchi” alisema Khatib huyo |