Monday, November 25

COSOTA KUSIMAMIA HAKIMILIKI YA SANAA ZA UFUNDI KATIKA MFUMO WA MAUZO KWA MTANDAO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akitoa maelekezo kwa COSOTA na BASATA kuandaa mfumo wa kuuza kazi za Wachoraji na Wachongaji kwa njia ya mtandao kufuatia ukuaji wa teknolojia na uwanda mpana wa masoko katika mfumo wa mtandao au  programu za  simu ’Apps’  leo Machi 15,2021 Jijini Dar es Salaam katika kikao wadau  wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kilicholenga  kutatua changamoto zinazowakabili.

Afisa Mtendaji  Mkuu  wa Taasisi ya Hakimiliki  na Hakishiriki Tanzania Doreen Sinare akiwasisitiza  wanachama wa Tingatinga Arts kusajili kazi zao badala ya kusubiri mpaka wanapopata changamoto ndiyo wanakumbuka kujisajili, katika kikao na wadau  wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji  kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam leo Machi 15,2021  kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.

Katibu wa Tingatinga Arts Tanzania Bw. … akiwasilisha akimwomba Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa kumsaidia kutatua changamoto ya mgogoro wa mipaka ya Kiwanja cha  Ofisi yao  Oysterbay leo  Machi 15,2021 jijini Dar es Salaam katika kikao wadau  wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kwa kilicholenga kutatua changamoto zinazowakabili.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa ameagiza COSOTA na BASATA kuandaa mfumo wa kuuza kazi za Wachoraji na Wachongaji kwa njia ya mtandao.

Mheshimiwa Bashungwa ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na Wasanii wa Sanaa ya Uchoraji na uchongaji nchini kilicholenga kutatua  changamoto Zinazowakabili katika uendeshaji wa kazi zao ikiwemo suala la masoko.

“Katika karne hii ya 21 suala la Masoko linafanyika kwa njia ya mtandao na njia hii ni rahisi na inatangaza biashara kwa haraka zaidi na katika hili COSOTA mtatakiwa kuhakikisha mnalinda Hakimiliki za kazi hizo,”alisema Mhe.Bashungwa.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Waziri huyo aliwasihi Wachoraji na Wachongaji kusajili kazi zao COSOTA ili ziweze kulindwa, pia alitoa msisitizo kwa wadau hao kuhakikisha wanawasiliana BASATA pamoja na COSOTA pale wanapokuwa na mikataba yao kibiashara kwa lengo la  kupata ushauri wa kisheria ili kuweza  kulinda kazi hiyo pamoja na maslahi yake.

Pamoja na hayo naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi.Doreen Sinare alieleza kuwa taasisi hiyo imetengeneza Kanuni mpya ambazo zitawasaidia

Wachoraji na Wachongaji kunufaika na kazi zao baada ya kuuza kazi zao na kazi hizo kwenda kuuzwa tena nje ya nchi kupitia minada na njia nyingine kama hizo ambapo kazi huuzwa kwa bei za juu ilihali msanii kutokupata chochote  kutokana  na mauzo hayo zijulikanazo kama ‘resale royalties rights’.

“Napenda kuwasisitiza kuhusu suala la kusajili kazi zenu kuna wakati nilitembelea ofisi za Tingatinga na nikawashauri kuhusu suala la kusajili kazi zenu COSOTA lakini baadhi yenu walikuja ila wengine hawakuja sasa naendelea kuwasisitiza kusajili msisubiri mpaka mnapopata changamoto ndiyo mnaanza kuhangaika,”alisema Bibi.Doreen.

Pamoja na hayo Mtendaji huyo alieleza dhamira  yake ya kutembelea eneo la biashara ya vinyago Mwenge Machi 19, 2021 kwa lengo la kuwapa elimu ya Hakimiliki na Hakishiriki ili kuwaongezea uelewa wa masuala hayo ikiwemo maboresho ya Kanuni mbalimbali zinazosimamia hakimiliki.

Pamoja na Kituo cha Wachoraji wa Sanaa ya Tingatinga Oysterbay ambapo itakuwa ni mara nyingine anawatembelea.

Mbali na hayo Bibi.Doreen alitangaza  napenda kutoa ofa kwa wanawake wanaofanya kazi ya Sanaa ya Ufundi kupamba Ofisi ya COSOTA kwa kazi zao   ikiwemo kwa Sanaa ya uchoraji au uchongaji Kufuatia mgogoro wa Tingatinga Arts na Kampuni ya Kenya Mtendaji Mkuu wa COSOTA aliwaelekeza viongozi wa chama hicho  kumpeleka  mkataba wao katika Ofisi yake ili aweze kutoa ushauri.

Pamoja na hayo Katika kikao Waziri Bahungwa alisisitiza mikataba huo ufuatiliwe na COSOTA, na kama kuna haki za Tingatinga basi haki hizo zifuafuatiliwe na zipatikane  hii ni kutokana na sintofahamu ya kusemekana kuwepo kwa baadhi ya wasanii ambao  walisaini na kulipwa kwa kazi hiyo. Hivyo mkataba ndio utatoa picha kamili.

Kwa upande Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw.Andrian Nyangamale alitoa ombi kwa Serikali kuwa anaomba katika zawadi zile za vinyago au picha za kuchorwa zinazotolewa kwa wageni Ikulu basi Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataje jina la aliyefanya fanya kazi hiyo pale anapokabishi. *Mh. Waziri alipokea na kuahidi kufanyia kazi jambo hilo.*