Sunday, November 24

Wanawake wanaweza, watizameni kwa jicho la maendeleo

Imeandikwa na Amina Ahmed – Pemba

Walio Wengi wanafikiria ya kuwa mwanamke hawezi  kusimama  na kugombea nafasi  ya uwongozi katika jimbo iwe ya Uwakilishi, Ubunge Udiwani na nyadhifa nyengine lakini, Kuelekea  Uchaguzi Mkuu  October 28 mwaka huu 2020 baadhi ya wanawake wameweza kuonesha ujasiri wa kugombea nafasi za uongozi  majimboni  licha ya awali  kukabiliwa na changamoto ya virusi vya korona huku ikiwa ni mara ya kwanza kuingia katika mchakato wa kugombea  .

Leo katika makala hii  maalum ya wanawake na uongozi  tutamuangalia  mjasiriamali mwanamke  alieamua kujitosa katika  Nyanja ya kisiasa na kufanikiwa   kugombea nafasi ya ubunge  katika jimbo la chake chake  Mkoa wa kusini Pemba kupitia chama cha cha wakulima  AAFP.

Ni Fatma Doto Shauri Mkaazi wa Madungu chake chake Pemba ambae ni mjasiriamali wa biashara ndogo ndogo za vyakula huku akiwa ni mama wa familia mume na watoto watano.

’’Mwanzoni mwa mwaka huu harakati zangu za kutaka kuingia katika mchakato wa kugombea ziliishia kichwani tu kutokana na hali ya maambukizi ya korona ilivyokua kwanza nilitetereka sana kiuchumi mimi na familia yangu kutokana na biashara ambayo inaniingizia kipato kwa aslilimia 90 wateja wake kuwa ni wanafunzi wa skuli’’ Alisema bi Fatma .

Mara baada ya hali ya maambukizi kupungua licha ya kua hali ya kiuchumi kwa mgombea huyo haikua sawa alisimamia msimamo wake wa kutaka kugombea uongozi na mara baada ya kipenga kupulizwa alijitosa kuiwania nafasi hiyo kwa hatua za awali za uchukuaji fomu .

Bi Fatma alianza harakati za siasa kwa kuomba ridhaa kupitia chama chake cha(AAFP) ya kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la chake chake baada ya viongozi wa chama hicho kujiridhisha kugombea nafasi hiyo.

Alisema‘’Kilichonishawishi kuigombea nafasi hii ni kutaka kuisaidia jamii ya wanachake chake katika Nyanja zote hususan ni wanawake wenzangu katika suala zima la ujasiriamali.

Wanajamii waliowengi hususan ni wale ambao wanamjua bi Fatma Shauri wanasema kutokana na ujasiri wa mwanamke huyu wanamatumaini makubwa endapo atafanikiwa kupata kura za kutosha kwani ni mama ambae amekua mchapakazi na mpenda mashirikiano na wanajamii .

”Sitoacha kumuunga mkono mwanamke mwezangu katika jambo hili aliloamua kwani ni wazi anamoyo wenye malengo mazuri kwa wanachake chake hususan ni kwetu akina mama kwa sababu hajawa kiongozi tunayaona mashirikiano yake kiatika harakati mbali mbali za ujasiriamali anatushirikisha mara leo katuita tutengeneze hiki mara kesho kakusanya wanawake kuwafundisha mbinu za ujasiriamali na ni kweli zinatusaidia tunaacha kua tegemezi tunajisaidia baadhi ya shida ndogo ndogo ”Alisema ashura Ali Abdallah ambae ni jirani wa karibu na mgombea huyo.

Bi fatma alianza kuingia katika harakati za kisiasa kwa chama cha wakulima mwanzoni mwa mwaka 2019 ambapo awali alikua si mwanachama wa chama chochote cha siasa bali ni mjasiriamali wa biashara ndogo ndogo za vyakula katika skuli ya madungu msingi sehemu mbali mbali zenye mikusanyiko ya watu.

Ameeleza kuwa awali suala la kugombea uongozi kwa upande wake halikuweza kuwa jepesi kutokana na kukatishwa tamaa na wanajamii ya kuwa mwanamke hawezi kuongoza. Lakini kwa sasa ameweza kujenga uthubutu kutokana na kuona mifano mizuri ya viongozi wanawake katika Nyanja mbali mbali na kuamua kuwa jasiri kupitia mifano ya wanawake hao akiwemo Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan ,Viongozi mbali mbali walioteuliwa na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Balozi Amina Salum Ali Dk Sira Ubwa Mamboya,Riziki Pembe Juma Shadya Mohammed ambao ni mawaziri na naibu waziri wanawake ambao utendaji wao wa kazi kwa bi Fatma Doto umekua ni kielezo cha kuiga kujiamini na kupata nguvu na ujasiri mda wote.

“Namshukuru sana mumewangu kwa mashirikiano ambayo ananionesha katika kuniunga mkono juu ya suala hili amekua msaada mkubwa sana hajawahi kunivunja moyo mpaka leo nimeweza kusimama kugombea “alisema mama huyo.

Fumu Yussuf Fumu ni mume wa bi Fatma Shauri anasema aliamua kumruhusu mke wake kujiingiza katika harakati za siasa ili kutomnyima kiu yake yakuikomboa jamii ya wanachake chake

‘’Mwanamke anaweza kua kiongozi mahali popote na maendeleo yakapatikana na kuna mifano mingi tu ya wanawake na wanaongoza vizuri na wanatimiza majukumu yao kama inavyotakiwa na mm nmeamuua kumuunga mkono juu ya suala hili ili aweze kuionesha jamii uwezo wake “.

Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa kanda ya pemba awali kabla mchakato wa kuanza kugombea kilikua mstari wa mbele katia katika kushajihisha kuona wanawake wanaitumia ipasavyo fursa ya kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kwa kuandaa mikutano ya shehia ya kuwajengea uwezo wanawake kwa kutoa elimu juu ya masuala ya uongozi .

Kuanzisha timu za wanaume kumi mabadiliko katika baadhi ya Maeneo kwa lengo kuwasaidia wanawake kuhamasika kugombea nafasi za uongozi.

Bi Fat hiya Mussa Saidi mratibu wa chama cha waandishi wa habari wanawake kisiwani pemba amesema chama hicho Bado kinaendelea kutoa mashirikiano kwa kuhamasisha wanawake kuchaguliwa majimboni.

Bi fatma shauri amewaasa wanachake chake kumuunga mkono katika uchaguzi mkuu kwa kumpigia kura nyingi za ndio ili aweze kusimama kuwa mbunge wa Chake Chake kwa lengo la kuwaletea maendeleo.