Na.Maulid Yussuf – WEMA Zanzibar.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema kuna umuhimu wa kuweka mikakati ya haraka ili kuweza.kujipanga endapo yatatokea majanga ya kitaifa na kusababishwa kufunga Skuli.
Katibu Mkuu Wizara hiyo bwana.Ali Khamis Juma amesema hayo wakati akichangia tathmini ya athari za kijinsia kwa.Wanafunzi katika kipindi cha kufungwa Skuli kufuatia mlipuko wa maradhi ya Korona mwaka 2020, katika ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini mjini Unguja.
Amesema ni lazima jitihada zichukuliwe na mapema ili kuweza kuwasaidia watoto kuweza kusoma kwa utulivu na kuwaepusha na.matatizo.mbalimbali yakiwemo ya mimba za.mapema.
Mapema akiwasilisha ripoti hiyo, Mkuu wa Seksheni ya Stadi za Maisha Kutoka Kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha Bi Fatma Mbarak Hashim amesema tathmini imeonesha kuwa jumla ya wanafunzi 69 wameacha skuli, wanafunzi 15 wamepata ujauzito, wanafunzi 2 ndoa za utotoni, wanafunzi 4 wa kike wamefanyiwa udhalilishaji wa kingono na wanafunzi 23 wamejiingiza katika ajira za utotoni.
Bi Fatma amesema, tathmini hiyo imepatikana kufuatia utafiti mdogo walioufanya katika Mikoa yote mitano ya Zanzibar kwa Skuli 15 zikiwemo 10 za Sekondari na 5 za msingi.
Amesema hali hiyo ni mbaya na bado elimu zaidi inahitajika kwa wanafunzi na.hata wazazi juu ya kutambua umuhimu wa kusoma pamoja na athari za matatizo hayo yaliyojitokeza katika kipindi hicho cha kufungwa Skuli, ili Taifa liweze.kuzalisha viongozi bora wa baadae.
Amefahamisha kuwa matatizo.hayo yameonekana kujitoteza kutokana na sababj mbalimbali ikiwemo watoto kuangalia picha zisizofaa katika simu na mitandao mbalimbali, pamoja na kushawishiana wenyewe kwa wenyewe.
Amesema Wizara ya.Elimu ilipozifunga Skuli ilikuwa na nia njema sana na.ndio maana ikaweka utaratibu wa.kuwapatia wanafunzi masomo kwa njia mbali mbali ili waweze kuwa na.kitu cha kuwashughulisha badala ya kufanya vitendo visivyo faa.
Nao washiriki wa Mkutano.huo wameiomba wizara kushirikiana.na.kitengo hicho kuhakikisha kwanza.wanawarejesha watoto 69 walioacha skuli, kwani ni idadi kubwa sana Taifa inaweza.kulipoteza.kutikana na sababu zisizokuwa na msingi.
Pia wameshauri Kuwa kupitia Idara ya Maafa kuhakikisha inaanza.kuweka mikakati ya mapema kwa.kutoa.elimu kwa jamii juu ya,majanga mbalimbali yanayowwza kujitokeza kuliko kusubiri tatizo litokee.