Na.Talib Ussi Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeeleza haitoweza kufanikisha mpango wake wa ajira laki tatu kuwa Bila ya Vijana madhubuti wenye siha na afya njema, akili timamu na walioelimika, pamona waliosalimika na dawa ya kulevya.
Hayo aliyaeleza Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Othman Masoud Othman huko Ocien view wakati akifungua kongamano la Madawa ya kulevya ambalo limeshirikisha wananchi wa mikoa mitatu ya Unguja pamoja na kamati za ulinzi na usalama.
Alisema ili kufikia mpango huo kuna haja ya kuwaokoa vijana na janga la matumizi ya madawa ya kulevya na kukuzaa ushiriki wao katika kujenga taifa kupitia sekta ya ajira
“Lakini hayo tutayafikia kama vijana wetu watakuwa na afya njema na uwezo wa kufanyakazi na hili tikishikrikiana linawezekana, “ alisema Makamu huyo.
Alisema kuwa ili vijana waweze kuwa warithi watakaokuja kuendeleza mipango, mikakati na malengo ya maendeleo ya Zanzibar kunahitajika ushiriki wao wa moja kwa moja katika miradi ya Uchumi wa Buluu nchini ambapo hilo hilo halitowezekana pasina afya na sia njema.
Alifahamisha kuwa dawa za Kulevya ni janga la Kimataifa, ambapo Zanzibanr haikunusurika kwani imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na tatizo hilo.
Alieleza kuwa Zanzibar inakisiwa kuwa na takribani ya watu 10,000 wanaotumia dawa za kulevya na kiasi kikubwa ya waathiriwa hao ni vijana.
“Idadi hii sio ndogo na athari yake ni kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria, kwani matumizi haya yanachochea maradhi mbali mbali ambayo hudhofisha nguvu kazi ya Taifa ambao ni vijana wetu” alisema.
Akifafanuwa athari za ziada zitokanazo na Madawa hayo Makamu huyo, kuwa matumizi ya madawa hayo husababisha maradhi mbali mbali ikiwemo, Kensa, magonjwa ya akili, maambukizi ya Ukimwi kufikia 5.1%, homa ya Ini B – 8.4% , Ini C – 15.1% sambamba maradhi ya kujamiiana yamefikia 0.2%,.
Makamu alibainisha kuwa hali hiyo inaonyesha kwa kiasi gani nguvu kazi ya vijana inavyoweza kupotea kwa kasi ndani ya visiwa vya unguja na Pemba na kuathiri uchumi wa Visiwa hivyo.
Kongamano hillo la siku moja limepanga kuwasilishwa mada tatu ikiwemo Mipango ya kuzuia na kupambana na uhalifu wa Dawa za Kulevya, Kuimarisha Kinga ya msingi dhidi ya Dawa za Kulevya pamoja na Kutatua changamoto za utumiaji na matendo ya Dawa za Kulevya.
“Ili tuweze kufanikiwa katika kuyatekeleza hayo, ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa mawazo yake juu ya mbinu bora zitakazosaidia kuleta matokeo chanya ikiwemo kuzifanyia kazi zile kesi za Dawa za Kulevya zinazochukua muda mrefu bila kumalizika, kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2009 na Sheria nyengine zinazofanya kazi pamoja” alisema Makamu.
Alisema kwamba endapo kila mmoja akitimiza wajibu wake katika kuyasimamia hayo kwa uzalendo na kwa uadilifu mkubwa itasaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Mfumo wa umoja wa kitaifa kujenga uchumi imara na kufikia malengo iliyojipangia kwani itaweza kupunguza gharama za kuwatibu vijana walioathirika na Dawa hizo.
Alisema azma ya Serikali ya Zanzibar ni kuona wananchi wake wanaishi katika maisha mazuri bila ya biashara wala matumizi ya Dawa za Kulevya.
Pia kwa upande mwengine alisema kuna jumla ya kesi 654 kwa mwaka 2018, kesi 503 kwa mwaka 2019 na kesi 454 kwa mwaka 2020 Kwa mujibu wa taarifa za polisi, na kueleza kwamba huo ni ushahidi tosha na kuthibitisha kuwa dawa za kulevya zinaingizwa nchini zanzibar.
Aliwaomba washiriki wa kongamano hilo pamoja na wananchi kwa ujumla kushiriki katika vita hivyo kwani wote ni wadau katika Mapambano ya dawa za Kulevya na siyo kuachia mtu mmoja au Taasisi moja.
Alisema vita ya Madawa ya kulevya ni kubwa mnoo na kufahamisha moja ya silaha zake ni mashirikiano ya pamoja kuanzia ngazi ya jamii ambae itahitajika kutoa taarifa za uhalifu hadi Mahkama ambayo itatoa maamuzi katika kesi hizo.
Akitoa neno shukrani makamu wa kwanza wa rais, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharbi, Idrisa Kitwana ameeleza iko haja ya kuiongezea makali sheria iliyopo kuendana na wakati