NA KHADIJA KOMBO-PEMBA
Unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi imetajwa kuwa ni moja kati ya sababu zinazopelekea kuwakosesha haki zao za msingi watu wa jamii hiyo.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hio Kisiwani Pemba bibi Awena Khamis Rashid wakati alikuwa akizungumza na Uongozi wa Jumuyiya ya Zanzibar International development ZIDO katika hafla fupi ya ugawaji wa sadaka kawa watu hao kutoka Jumuiya hio huko katika ukumbi wa Skuli ya Madungu Sekondari Chake Chake.
Amesema watu wenyeulemavu wa ngozi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi mbali na unyanyapaa lakini pia hata upatikanaji wa haki ya elimu bado kwao ni changamoto.
Naye Mkuu wa Jumuiya ya ZIDO kwa upande wa Zanzibar ndugu Makame Ramadhani amesema kutokana na changamoto hizo Jumuiya yao itahakikisha inawasaidia watu hao kila hali itakapo ruhusu.
Jumuiya ya ZIDO ambayo iko chini ya Rais wake Bibi Rehana Merali kutoka Canada kwa hapa Zanzibar Makao makuu yake yapo Makunduchi na imekuwa ikitoa misaada ya vitu mbali mbali kwa wananchi wa Zanzibar kila ifikapo Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI