Thursday, January 16

NGO’s zatakiwa kutambua wajibu wao kwa jamii.

MTANDAO wa Asasi za kiraia Pemba (PASCO) umezitaka NGOs Kisiwani humo, kutokujiingiza katika masuala ya kisiasa badala yake kutambua wajibu wao katika kusaidia jamii.

Hayo yameelezwa na katibu Mkuu PASCO Sifuni Ali Haji, wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kupitia uwasilishwaji wa Rasimu ya Mswaada wa sheria ya jumuiya zisizo za kiserikali, uliofanyika mjini chake chake.

alisema sio jambo jema kwa wanajumuiya za asasi za kiraia kujishuhulisha na mambo ya kisiasa, katika kipindi hiki cha uchaguzi badala yake kujuwa majukumu yao katika jamii.

Aidha aliwataka wanajumuiya kuhakikisha wanafuata sera, sheria na kanuni za jumuiya zao katika kuwasaidia wananchi, katika kuwapatia maendeleo.

Akizungumzia kuhusu uwasilishwaji wa Rasimu ya Mswaada wa Sheria ya jumuiya zisizo za kiserikali, alisema sababu kubwa ni sera na sheria zote zimeshapitiwa na muda, kulingana na wakati huu wa sasa.

“Hapa jumuiya zimepata nafasi ya kuipitia makini Rasimu hii ya sheria, na kutoa mapendekezo yao ili kuona sheria inayokuja inakwenda sambamba na matakwa ya NGOs na Serikali”alisema.

Katibu Sifuni alisema asasi za kiraia zinamchango mkubwa kwa serikali, kwani ndio zinazofanya kazi moja kwa moja na jamii, hivyo alizitaka kubadilika na kwenda kisasa zaidi kulingana na maendeleo ya sasa.

Kwa upande wake mrajisi wa asasi za kirai Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla, alizitaka jumuiya kubadilika kufanya kazi kwa vitendo zaidi baada ya kufanya usajili wake.

Alisema serikali itaendelea kufanya kazi pamoja na NGOs, kwani imetambua mchango mkubwa wa taasisi hizo kwa jamii katika kuwsaidia wanajamii.

“kumekua na wimbi kuba la jumuiya kusajiliwa, kuanzia Januari tunaanza ukurasa mpaya hapa tutazijuwa jumuiya ambazo zipo hai na zilizokufa,kila jumuiya lazima kuwasilia ripoti yake ya fedha kwa mrajisi wa NGOs, Kwa upande wake mrajisi wa asasi za kirai Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla, alizitaka jumuiya kubadilika kufanya kazi kwa vitendo zaidi baada ya kufanya usajili wake.

Alisema serikali itaendelea kufanya kazi pamoja na NGOs, kwani imetambua mchango mkubwa wa taasisi hizo kwa jamii, katika kusaidia jamii.

“kumekua na wimbi kuba la jumuiya kusajiliwa, kuanzia Januari tunaanza ukurasa mpaya hapa tutazijuwa jumuiya ambazo zipo hai na zilizokufa,kila jumuiya lazima kuwasilia ripoti yake ya fedha na utekelezaji kwa mrajis wa NGOs”alisema.

Mratib wa NGOs Pemba Halima Khamis Alio, aliishukuru PASCO na Foundation For Civil Socety kwa kuandaa mkutano huo wa kupitia rasimu ya Mswaada wa sheria ya jumiya zisizo za kiserikali.

Wakichagia katika mkutano huo kwa niaba ya makundi yao, Safia Saleh Sultani aliitaka ofisi mrajis wa NGOs, kuhakikisha baada ya rasimu hiyo kupita kuwa sheria kamili, vizuri kuziwasilisha katika NGOs mbali mbali ili kuzifahamu vizuri.

Siti Habibu Mohamed alitaka ofisi ya mrajis kupunguza muda wa usajili wa NGOs, kwa usajili unachukua muda mkubwa.