Monday, November 25

UN: Vifo 745,000 vimetokona na kufanya kazi sana

Utafiti wa Shirika la Afya duniani (WHO) na la Kazi duniani (ILO) unaonesha kufanya kazi kwa muda mwingi katika kipindi cha mwaka 2016, kumechangia vifo 745,000.

Katika utafiti wao huo, mashirika WHO na ILO kwa pamoja yanakadiria watu 398,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa kiharusi na 347,000 magonjwa ya moyo kwa 2016.

Sababu ambayo inaoneshwa ni kufanya kazi kwa muda mrefu kunakofikia masaa 55 kwa wiki.

Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya vifo vilivyotokana na magonjwa ya moyo kwa sababu ya kufanya kazi kwa muda mrefu viliongezeka kwa asilimia 42, na kiharusu asilimia 19, na mzigo mkubwa wa vifo hivyo kwa asilimia 72 unabebwa na wanaume.

Maeneo ambayo yanatajwa kuwa na athari zaidi  kwa wafanyakazi wa umri wa kati au wazee ni Magharibi mwa Asia Pasifiki na Ukanda wa Kusini-Mashariki mwa Asia.

Masaa ya kufanya kazi yanapaswa kuwa masaa 35 hadi 40. Profesa Jian Li mmoja kati wa maafisa waandamizi wa WHO, walioshiriki utafiti huo anasema;

“Tumebaini kwamba, kufanya kazi kwamasaa 55 au zaidi kwa wiki, kuonaongeza hatari ya kufa kwa magonjwa haya ya moyo kwa asilimia 17, baada ya miaka 10. Hilo limejikita katika takwimu za washiriki 340,000 za makundi ya tafiti 22 tofauti duniani. Vilevile tumebaini kufanya kazi kwa masaa 55 au zaidi kwa wiki kuonaongeza hatari ya kupata kiharusi kwa asilimia 35,” Profesa Jian Li