Saturday, October 19

UVCCM wampongeza DK. Mwinyi.

KATIBU wa Umoja wa Vijana Tawi la Kichungwani Hashil Fadhil Abdulla, akizungumza katika kikao cha kumpongeza Dk.Mwinyi kilichofanyika katika tawi la UVCCM Kichungwani Wilaya ya Chake Chake .(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Kichungwani Wilaya ya Chake Chake, wamempongeza Dk.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa kuchaguliwa kwake huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkono katika utendaji wake wa kazi.

Umoja huo umesema Dk.Mwinyi ni kiongozi shupavu na mchapakazi, hivyo watendaji watakaoteuliwa wanapaswa kwendana na kasi yake ya uongozi katika kuijenga Zanzibar mpya yenye maendeleo.

Hayo yameyaeleza na viongozi wa UVCCM Tawi la Kichungwani mjini Chake Chake, wakati alipokuwa katika kikao cha pamoja na vijana wao, cha kujipongeza baada ya kuiweka CCM Tena madarakani.

Katibu wa UVCCM Tawi la Kichungwani Hashil Fadhil Abdulla, alisema dunia nzima inafahamu juu ya ushindi wa Dk.Mwinyi, hiyo inatokana na ufanyaji wake wa kampenzi za kisayansi na wananchi kuzikubalia.

Alisema kwa sasa vijana wanatarajia mambo makubwa kutoka kutoka kwa viongozi wao, hivyo watahakikisha wanakuwa bega kwa began a viongozi wao.

“lengo ni kuwapongeza viongozi kwa ushindi mkubwa walioupata katika kampeni, sisi vijana tutakua nao bega kwa bega ili kufikia malengo yaliokusudiwa”alisema.

Waliwataka vijana kuacha kufanya kazi kimazowea na badala yake kujiweka tayari kwenda na kasi ya mabadiliko ya Dk Mwinyi, ufanyaji wa kazi wa miaka 64 iliopita hivyo kasi ya 2020/2025 itawaacha nyuma.

Naye Hassan Khamis Hamad UVCCM Kichungwani, aliwashukuru viongozi wa mkoa wa kusini kwa kuimarisha ulinzi ndani ya mkoa huo, katika kipindi chote cha uchaguzi, huku kukuwa na ishara kwa wapinzani ndani ya kisiwa cha Pemba inaanza kufutika.

Kwa upande wake Zadida Abdalla Rashid, aliipongeza kamati maalumu ya CCM ya Mkoa wa kusini kuandaa mikakati maalumu ya kuhakikisha CCM inashinda, pamoja na kuwalea vijana na kuhakikisha wanashinda uchuzi mkuu uliopita.

Alisema vijana wa kichungwani wanaimani na viongozi walioshinda kwani wakati umefika kwa viongozi hao wamajimbo kuwaangalia vijana kwa jicho la hura.

Naye Abdulhalim Hamad Ali katib wa wadi ya madungu, aliwapongeza viongozi wote wa Tanzania kwani wanaimani wao katika kuongoza vizuri nchi, huku akiwataka vijana wenzake kusheherekea ushindi huo bila ya kuwaudhi wenzao.

Katibu mwenezi wa tawi la Kichungwani Bahati Mohamed Haji, aliwataka vijana wa ccm kutokurudi nyuma badala yake kushirikiana katika ujenzi wa Zanzibar mpya.

KATIBU Mwenezi wa Tawi la UVCCM Kichungwani Wilaya ya Chake Chake Bahati Mohamed Haji, akizungumza na vijana wa UVCCM Tawi la Kichungwani katika hafla ya kumpongeza Dk.Mwinyi, hafla iliyofanyika katika Tawi hilo Kichungwani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)