NA ABDI SULEIMAN.
VIONGOZI wa shehia za Pemba, wameshauriwa kusikiliza changamoto zinazowakabili wanachi hususana wanawake katika shehia zao, juu ya suala la umiliki wa ardhi, ili kuepusha usumbufu unaowakabili katika suala la ardhi.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa KUKHAWA Pemba Hafidh Abdi said, wakati akizungumza na masheha wa wilaya ya micheweni wakati wa mkutano wa kutoa elimu juu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake wa wilaya hiyoo.
Hafidhi alisema masheha ni viongozi, wenye uelewa mkubwa wa kuzitatua na kuzisemea changamoto, zinazowakabili wananchi katika masuala ya ardhi na umiliki wake.
Alisema Wanawake wengi wamekuwa wakishindwa mbele ya wanaume, kumiliki ardhi kutoka na changamoto mbali mbali ikiwemo, mfumo dume hata katika jambo la mirathi hali inayowafanya wanawake kunyimwa kumili mali ikiwemo ardhi.
”Wananchi wanaweza wasijue ardhi ipi huru na ardhii ipi ni mali ya serikali, lakini nyinyi masheha mnajua hilo muwasaidie wanachi katika hili, kwa kusikiliza changamoto na kujuwa nini kinawakwamisha mpaka wanawake hawamiliki ardhi”alisema.
Mwenyekiti wa mradi wa haki ya umiliki wa ardhi Pemba, unaoendeshwa na Jumuiya ya KUKHAWA Zuleikha Maulid Kheir, amewataka masheha kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu juu ya ardhi za serikali, ambazo zipo katika shehia zao ili kufuatilia na kuziomba ardhi hizo kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
“Wapo Wanawake wanatamani kumiliki ardhi kwa ajili kufanya manunuzi, pamoja na kuziendeleza kimaendeleo wamekuwa wakizikosa kutokana na masheha, kutozitolea taarifa ardhi hizo za serikali kwa taasisi husika”alisema.
Akiwasilisha mada kwa masheha hao Afisa kutoka kamisheni ya ardhi Pemba, Asha suleiman said alisema endapo wananchi watafuata sheria za ardhi, zilizowekwa katika kumiliki ardhi zitasaidia kuepuka migogoro isiyo ya lazima.
“Wananchi wamekuwa wakiingia katika migogoro ya ardhi na wanawake wamekuwa wakikosa kumiliki ardhi, kutokana na kutojua sheria zilizowekwa katika umiliki wa ardhi, mwanachi anahaki ya kumilki ardhi ikiwa ni kwa mirathi, kupewa zawadi, kununua na nyenginezo, lakini kutokana na kutofuata sheria wanakosa haki zao wanawake na kuingia katika migogoro,”alisema.
Akitoa elimu ya kisheria juu ya suala la umiliki wa ardhi Mwanasheria Khalfan Amour Mohammed, aliwaasa masheha na
wananchi kutofautisha sheria za dini na sheria zilizowekwa na serikali, katika kumiliki ardhi kwa wanawake.
Alisema sheria ya dini imetofautiana na sheria ya serikali katika umiliki wa ardhi kwa wanawake, hususani katika suala la mirathi lakin sheria zote hizo, hazijamnyima Mwanamke fursa ya kutomiliki ardhi.
“Tatizo kubwa lililopo kisiwani hapa wanaume katika familia wanakataa kufanya mirathi, kwa mujibu wa sheria na kusababisha kumnyima ardhi mwanamke”alisema Khalfan.
Kwa upande wao Masheha wa wilaya hiyo, wameiyomba kamishenia ya ardhi Pemba, kutembelea na kujitangaza katika shehia zao na kutoa elimu juu ya umiliki wa ardhi na kuondosha usumbufu wanaoupata wananchi.
Sheha wa shehia ya Tumbe mshariki Massoud Khamis Hamad, aliwaomba mashehe wanaosimamia masuala ya mirathi kutoka ofisi ya wakfu pemba, kutoa elimu kwa masheha wanaoaminika kwa jamii na kuwapa elimu ya mirathi, ili kuwasaidia kutatua kesi hizo zinapotokea katika shehia