Sunday, November 24

MH. Hemed: SMZ imefarijika kwa mafanikio ya vikao vya Sektarieti ya Kitaifa ya kujadili hoja na Changamoto za Muungano.

Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla akisisitiza msimamo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kusimamia utatauzi wa zile kero zilizomo ndani ya Muungano ambazo tayari zimeshapatia muelekeo wa utatauzi.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza na, Viongozi wa Sekretarieti ya Kitaifa inayojadili changamoto za Muungano liofika Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.
Baadhi ya Maafisa wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walioshiriki mazungumzo hayo.
Viongozi wa Sekretarieti ya Kitaifa inayojadili changamoto za Muungano wakipiga kofi na kushangiria kauli ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla aliyopitoa wakati wa mazungumzo yao.

Picha na – OMPR – ZNZ.

 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefarijika kwa mafanikio ya vikao vya Sektarieti ya Kitaifa ya kujadili hoja na Changmoto za Muungano, ambapo  jumla ya changamoto nane zinatarajiwa kutatuliwa katika kipindi kifupi kijacho.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, ameyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Sektarieti ya Kitaifa inayojadili changamoto za Muungano, iliofika Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Mheshimiwa Hemed, amesema mashirikiano mazuri  yaliyopo baina ya Ofisi yake, pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, ni kutokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, aliyowapa watendaji wakuu chini ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunano wa Tanzania, Mheshimiwa Philip Isdor Mpango.

Aidha amemshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mashirikiano yake , hali ambayo yeye pamoja na ofisi yake imekuwa ni kiungo kikubwa katika kuhakikisha mashirikiano ya pamoja yanapatikana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, amesema Serikali ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar awamu ya nane, chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dr Hussein Ali Mwinyi, imesisitiza kutatuliwa kwa changamoto hizo kwa maslahi ya wanancji wa Zanzibar na watanzania kwa ujumla.

Mapema Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungno na Mazingira Bi Merry N. Maganga, pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tixon T. Mzonda kwa pamoja wamemuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Sekretariti hiyo ipo inaendelea na vikao vyake ikiwa ni muendelezo wa kujadili na kuzipatia ufumbuzi hoja na changamoto zilizomo ndani ya Muungano.

 

 

Kassim Salum Abdi

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar