Monday, November 25

RAIS MSTAAFU MHE.DKT.JAKAYA KIKWETE AONGOZA KONGAMANO LA MIAKA 40 YA JUMUIYA YA SADC

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Maendeleo ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC lililofanyika katika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. william Anangisye akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Maendeleo ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC lililofanyika katika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Spika wa Bunge Mstaafu Mhe.Anna Makinda akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Maendeleo ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC lililofanyika katika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Maendeleo ya Jumuiya ya Kusini mwa Afrika SADC lililofanyika katika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Raisi Mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete ameongoza kongamano la maadhimisho ya miaka 40 ya maendeleo ya jumuiya ya kusini mwa Afrika SADC na kutoa uzoefu wa Tanzania.

Raisi Mstaafu Jakaya Kikwete alisema lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya ya SADC kupunguza utegemezi, kukuza ushirikiano utakaojenga utengamano wa kikanda,kuhamasisha utekelezaji wa sera ikiwa ni pamoja na kuchukua harua za pamoja katika kupata misaada kwa nchi za kimataifa.

“Maadhimisho haya yanaadhimishwa na Nchi zote Nchi wanachama wa Jumuia ya Nchi za SADC kuangalia malengo na mchango kutambua fursa zilizopo katika kuinua Uchumi “alisema Dkt Kikwete.

Hata hivyo alisema Wapigania uhuru kutoka Nchi nyingi za Afrika wanaendelea kuikumbuka Tanzania na kutokana na Hayati Rais Mwalimu Juliusi Nyerere baada ya Tanzania kupata uhuru hakuridhika kuona nchi nyingine zinateseka na wakoloni hivyo aliamua kujitolea kusaidia kwa kuwapatia maeneo Tanzania kuja kujifunza mbinu za kupambana na Wakoloni.

Kwa upande wake Spika wa bunge Mstaafu Mhe.Anna Makinda alisema wakati  baadhi ya wapiganaji waliokuwa wamekuja kupata mafunzo walipitia changamoto nyingi kwani wakisikia tu usafiri wa angani wowote unapita au kutua walimu walikuwa wanawaambia wakimbie wajifiche ili wahifadhi maisha yao wakihofia wakoloni kutoka nchi hizo zilizokuwa zinasaidiwa kuja kuwadhuru.

“Nchi nyingine zinakiri zenyewe isingekuwepo Tanzania Ukombozi wa baadhi za Afrika zingechelewa kupata uhuru ikiwemo Afrika Kusini ambayo uhuru wake walimwaga damu”alisema Mhe.Makinda.

Pamoja na hayo Mhe.Makinda alisema kuwa Hayati Mwalimu Julius Nyeyere na Rais wa lesotho Leoban kaunda wataendelea kukumbukwa kwa mchango wao mkubwa wa kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ya SADC ambayo walitoa mchango mkubwa.