KATIKA miaka ya hivi karibuni Dunia imekuwa ikishuhudia magonjwa mbali mbali kujitokeza, yapo yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa Duniani, pia yapo yanayotokana na wanyama moja kwa moja.
Katika magonjwa hayo yapo yanayotibika kwa Chanjo, pia yapo ambayo hadi sasa chanjo yake imeshindikana kupatikana, zaidi ya kutumia dawa ili kupunguza nguvu ya virusi vya ugonjwa huo.
Zoonosis ni ugonjwa ambao huambukizwa kutoka kwa wanyama wenye utu wa mgongo kwenda kwa mwanaadamu, ambapo kuna aina zaidi ya 200 ya magonjwa hayo, Zoonoses inajumuisha asilimia kubwa ya magonjwa mapya na yaliyopo kwa wanaadamu.
Vimeelea vya Zoonosis vinaweza kuwa ni baktiria, Virusi au vimelea vyengine, yapo magonjwa yanayoweza kutibika kwa chanjo kwa 100%, ikiwemo kichaa cha mbwa.
Kampeni ya elimu ya kunawa mikono, baada ya kuwasiliana na wanyama na marekebisho mengine ya tabia, zinaweza kupunguza kuenea kwa jamii kwa uogonjwa Zoonosis wakati unapotokea.
Watu wanaoishi karibu na maeneo ya jangwa au katika maeneo ya mijini na idadi kubwa ya wanyama wa porini, wako katika hatari ya kupata magonjwa kutoka kwa wanyama kama panya, mbweha au viboko.
Inakadiriwa asilimia 60% ya magonjwa yote tunayoyatambua duniani, hivi sasa yana asili ya kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Baadhi ya magonjwa ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binaadamu, ni VVU, SARS, Ebola, mafua ya ndege (H5N1), CORONA, kichaa cha mbwa hichi hakiwezi kumuambukiza mwengine (Rabis), Leptopspirosis.
Akiwasilisha mada, juu ya Uhusiano uliopo kati ya masoko ya wanyama na kusambaa kwa magonjwa mtambuka yanayotoka kwa wanyama (Zoonotic Diseases), Afisa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dk. Iddi Lipende, amesema asilimia 75% ya magonjwa yanayoibuka yameunganishwa na wanyamapori.
Amesema, kutokana na huku akiwashauri wananchi kukaa mbali na maeneo ya wanyama, pamoja na kuachana na tabia ya ulaji wa wanyamapo sambamba na unywaji wa maziwa mabichi ya wanyama.
“Katika hayo ni miongoni mwa magonjwa yaliyoibuka hivi karibuni, ni katika magonjwa yaliyokuwepo yakapotea na yakaibuka tena na yanakuja kwa kasi kushambulia dunia,”amesema.
Katika miaka ya hivi karibuni, wananchi wamekuwa wakishiriki kwa kiasi kikubwa katika ulaji wa wanyamapori, hususani watu wa vijijini wanaona ndio ubadilishaji wavyakula, kama vile panya, punda, nyati na nyani ulaji huo unasogeza karibu magonjwa ya wanyama kwenda kwa binaadamu.
Niwakati sasa kwa waandishi wa Mazingira kujikita katika kuelimisha jamii, juu ya madhara ya ulaji wa wanyama pari na maziwa mabichi yanayotoka kwa wanyama, ili kuepuka kupata maradhi mbali mbali yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binaadamu.
Lipende amesema mashirikiano ya pamoja kutoka taasisi mbali mbali ikiwemo JET, TAWIRI na Wizara ya Afya ili kuelimisha jamii juu ya madhara ya ulaji wanyamapori pamoja na kuishi karibu na wanyama.
“Serikali na mashirika mbali mbali kushirikiana katika kuweka kinga na taarifa ya kujinga kwa wananchi, kuachana na mila za kunywa damu, maziwa ambayo hayajachemshwa ambayo yanaweza kulea magonjwa ambayo hayajatambulika”aliongeza.
Madhara hayo hayakuwacha nyuma wazazi, katika kufuga wanyama majumbani kuwa makini na watoto wao wanapokuwa na wanyama wa majumbani, kuhakikisha wanapatia chanjo za mara kwa mara pamoja na kupatiwa dawa za minyooo mara kwa mara.
Kwa upande wa sababu inayopelekea kuongezeka kwa magonjwa hayo, anafahamisha kwamba ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu duniani hivi sasa, ikiwemo kuishi katika maeneo ambayo wanyama walikuwa wakitumia kama malisho na makaazi yao miaka ya nyuma na sasa kuwa makaazi ya binaadamu.
“myama kama tembo anaweza kukumbuka sehemu ambazo alikuwa wakipita tokea wadogo, sasa hili limekuwa taatizo katika njia nyingi za kupitia wanyama, zimekwua ni sehemu za kulimia mazao au makaazi ya watu, sasa wanyama wanarudi katika maeneo yao ya zamani”alisema.
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya taifa ya mipango ya matumizi ya ardhi Tanzania, Dr. Stephen Nindi anasema lengo kubwa la tume hiyo ni kuhakikisha matumizi ya rasilimali za ardhi yanakuwa endelevu na sahihi.
Tanzaia ina hifadhi ya taifa 21, ambapo kwa sasa wanaandaa mipango kwa nchi nzima kwenye hifadhi ya taifa na wanajaribu kuondosha kabisa migogoro ya ardhi nchini.
Amezitaja baadhi ya sheria ambazo zinahusiana na masuala ya wanyamapori, ni pamoja na Sheria ya Ardhi, Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Sheria ya Misitu, Sheria ya Rasilimali za Maji na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa JET Dr Ellen Otaru, aliwashukuru waandishi hao wa habari kwa ushiri wao, pamoja na kuwataka kuendelea kuelimisha jamii juu ya masuala mbali mbali ya umuhimu wa uhifadhi wa wanyama nchini.
Nao waandishi wa habari za mazingira walipongeza Chama hicho kwa kuwaandalia mafunzo hayo, ambayo ni muhimu kwao kwani yataweza kuwasaidia katika uwandishi wa habari zao za mazingira na kwani suala la mazingira lina uwanja mpana.
Tanzania ni makao makuu ya bianuwai kubwa ulimwenguni, iliyowekwa kati ya juu nchi zilizo katika ukanda wa kitropiki Afrika, kwa suala la maeneo tofauti ya ikolojia na katika spishi za aina ya endemism (URT-GEF-UNDP,2010).
Kwa
“Tathmini pana iliyoongozwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), inayoungwa mkono na Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS), imeonyesha kumbukumbu ya barabara 31 za wanyamapori nchini Tanzania (TAWIRI,2009), huku pango wa simamizi wa Tembo wa 2010 (TAWIRI,2010) ulibaini zaidi korido 25 zinazotumiwa na tembo, ambazo zingine hazikujumuishwa
Utafiti wa TAWIRI wa 2009”alisema.
Idadi ya watu wa Tanzania inatarajiwa kuongezeka kutoka kwa watu milioni 55 mnamo 2016 hadi milioni 138 mwaka 2050, wengi wanaishi vijijini takwimu za ukuaji ni kubwa zaidi katika maeneo kama magharibi mwa Tanzania.
Utafiti huo pia umebaini kuwa asili ya mwongozo wa Asali (HGF), TRIAS, TNC, AWF imefanya kazi na jamii katika Manyara Ranch – Ziwa Natron na barabara za Tarangire-Makuyuni kutoa sehemu salama kwa wanyama wa porini na ardhi kwa mifugo.
Mwandishi wa habari Felix Mwikyembe amesema ni wakati kwa waandishi wa habari kuelimisha jamii juu ya magonjwa mtambuka yanayotokana na zoonotic/zoonoses ambayo yanatoka kwa wanyama kwenda kwa binaadamu.
“Kama jamii itakuwa na elimu tosha juu ya magonjwa hayo, basi hata ufugaji wa wanyama mitaani utaweza kupungua, ili kujikinga na magonjwa ya wanyama”amesema.
Mwenyekiti wa JET Dr Ellen Otaru, amesema jamii bado inahitaji kutumia ardhi, kwa umakini ili na wanyamapori nao kuweza kutumia, kwa tumia mbinu mbali mbali, ikiwemo kufuga nyuki na vyura, wanaweza kutumika kulinda mashamba na wanyama wasiweze kuathiri kilimo.
Chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Marekani(USAID-Protect), chini ya mradi unaolenga kutoa elimu ya kutokomeza ukatili na ujangili kwa wanyamapori nchini, JET kuwa mstari wa mbele kutetea masuala yote ya uhifadhi wa wanyamapori na umuhimu wa kulinda bayonuai zake ikiwemo miti.
WHO inafanya kazi na Serikali za kitaifa, wasomi, mashirika yasio ya kiserikali na mashirika ya uhisani na washirika wa kikanda na kimataifa kuzuia na kudhibiti vitisho vya Zoonotic na athari zao kwa afya ya umma.
Athari zakijamii na kiuchumi huku jitahada hizo ni pamoja na kukuza ushirikiano wa kisekta katika kiunganishi cha mazingira ya binaadamu na wanyama katika sekta tafauti zinazohusika katika ngazi za kikanda, kitaifa na kimataifa.
Wataalamu wa utunzaji wa mazingira wamesema idadi ya wanyama, ndege na samaki duniani imepungua kwa zaidi ya theluthi mbili mnamo kipindi cha miaka 50 iliyopita, kutokana na matumizi ya binadamu yaliyokithiri.
Katika ripoti ya wataalamu hao iliyochapishwa Alhamisi ya Septemba 11, wamesema binadamu wameharibu robo tatu ya eneo la nchi kavu na asilimia 40 ya bahari, na wameonya kuwa kiwango hiki cha uharibifu wa mazingira kitakuwa na athari zisizoelezeka kwa afya za binadamu na maisha kwa ujumla.
Ripoti hiyo ijulikanayo kama Faharasa ya Sayari Hai ya mwaka 2020, imesema ufyekaji wa misitu na kilimo ni shughuli mbili zilizoongoza kuangamiza asilimia 60 ya viumbe hai kati ya mwaka 1970 na 2016.
Nusu karne iliyopita, imetahadharisha ripoti hiyo, imeshuhudia maendeleo makubwa kiuchumi, ambayo yameambatana na mahitaji makubwa ya rasilimali asilia.
EMAIL:abdisuleiman33@gmail.com
0718 968 355