Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar-Utawala/Taaluma Dk,Zakia Mohamed Abubakar akitoa hotuba ya makaribisho kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) Lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)Kampasi ya Maruhubi Zanzibar.
Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Hemed Suleiman Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) Lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)Kampasi ya Maruhubi Zanzibar.
Baadhi ya Wageni Waalikwa waliohudhuria katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) Lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)Kampasi ya Maruhubi Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI /MAELEZO ZANZIBAR.
Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka washiriki wa kongamano la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afika (SADC) kujadili kikamilifu mafanikio na changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo .
Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya miaka arobaini ya SADC huko katika ukumbi wa Kampasi ya Suza Maruhubi Mhe. Hemed amesema ni vyema kuangalia mafanikio ya SADC yalivyosaidia maendeleo ya nchi na jinsi yakujikwamua kutokana na changamoto kwa ustawi wa wananchi.
Alisema kuwa katika kujadili fursa ya Zanzibar ndani ya SADC katika Kongamano hilo ni vyema washiriki kuchambua na kuonyesha jinsi Zanzibar inavyoweza kutekeleza na kuimarisha kipaumbele cha Uchumi wa Bluu kupitia Jumuiya hiyo.
Aidha alisema kuna fursa nyingi za kibiashara katika nchi za SADC ambazo zikitumika vizuri zitaisaidia Zanzibar kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kipindi kifupi.
Alisisisitiza kuwa kongamano hilo lijikite katika kuchambua kwa kina jinsi Zanzibar itakavyonufaika kwa lugha yake ya Kiswahili kupitia Jumuiya hiyo na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa inayouzika katika nchi za SADC.
Alisema Zanzibar ikijipanga vizuri itawasaidia Vijana wengi waliohitimu taaluma ya lugha ya Kiswahili kuwapatia fursa za ajira ya kufundisha Kiswahili kama lugha ya pili katika nchi zinazounda Jumuiya hiyo.
Nae Balozi Soud Masoud Balozi amewataka wananchi wa Zanzibar kutumia fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zinapatikana katika Jumuiya ya SADC ili kuondokana na umasikini.
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeanzishwa 1 april,1980 huko Lusaka nchini Zambia na ina wanachama ndani ya nchi 16.