Tuesday, November 26

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MCHEZAJI WA KIMATAIFA WA TIMU YA CRYSTAL PALACE IKULU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza azma ya MchezajiwatimuyampirawamiguuwaKlabuya Crystal Palace inayoshirikiligikuuyaUingereza (EPL) MamadouSakhoyakuanzishakituo cha kuendelezavipajivyamichezokwavijanahapa Zanzibar.

 

Rais Dk. MwinyialitoapongezihizoleoIkuluJijini Zanzibar  wakati alipokutana kufanya mazungumzo na Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Kilabu ya  Crystal Palace inayoshiri kiligi kuu ya Uingereza (EPL) ambaye pia ni Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho.

Katika mazungumzo hayo, Rais Dk.  Mwinyi alieleza kwamba azma hiyo ni mwanzo mzuri katika kuinua na kuendeleza vipaji vya michezo vya vijana wa Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alimpongeza Mamadou kwa kuitembelea Zanzibar kwa mara ya pili kutokana na mazingira pamoja na watu wa Zanzibar na utamaduni wao.

Aidha,  Rais Dk. Mwinyi alimueleza mchezaji huyo wa timu ya Crystal Palace kuwa Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar iko tayari kushirikiana nae katika kuanzisha kituo hicho cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa  Zanzibar.

Rais Dk. Mwinyi alimueleza mchezaji huyo kuwa ujio  wake una umuhimu mkubwa katika kuutangaza utalii wa  Zanzibar pamoja na vivutio vilivyopo.

Nae Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Kilabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL)  ambaye pia ni Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho alimueleza Rais Dk. Mwinyi azma yake ya kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa Zanzibar.

Mamadou ambaye amefuatana na Mkewe Majda Sakho, alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo ya kuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana hapa  Zanzibar kwa kutambua kwamba anadeni na wajibu mkubwa wa kuleta maendeleo Afrika akijuwa kwamba yeye ni Mwafrika licha ya kuwa amezaliwa Ufaransa na anabeba uraia wa Taifa hilo.

Aliongeza kuwa ameichagua  Zanzibar  kuwa nieneo maalum kwa kuanzisha kituo hicho kitakachoendeleza soka hapa nchini.

Alisema kuwa vipaji vitakavyotolewa katika kituo hicho itakuwa ni alama maalum aliyoiacha katika kuinua soka nakuithami ni asili yake. “Ninapokuwa Ulaya sio wengi wanaoniuliza unatoka nchi gani ya Ulaya bali huniuliza ninatoka nchi gani ya Afrika, najivunia asili yangu ya Afrika, hivyo nimeamua kuifanyia kitu na nimeichagua  Zanzibar”,alisisitiza Mamadou

Sambamba na hayo,  Mamadou alieleza jinsi alivyovutiwa na mazingira na anavyoipenda Zanzibar kutokana na ukarimu wa watu wake, mazingira pamoja na utamaduni wake.

Mchezaji huyo pia, alieleza azma yake ya kujifunza lugha ya  Kiswahili na kueleza kuwa tayari ameshaanza kujifunza na kumueleza Rais kwamba mara ijayo atakapokuja basi atazungumza kwa lugha ya Kiswahili.

Baada ya kuzungumza na Rais Dk. Mwinyi, mchezaji huyo pia alipata fursa ya kufanya mahojiano na waandishi wa Habari waliohudhuria katika mazungumzo hayo ambapo katika maelezo yake amelezea utayari  wake wa kuwa Balozi wa Hiyari wa Kuutangaza Utalii wa  Zanzibar.

Nae Waziri Utalii na Mambo ya Kale Leila Muhamed Mussa alisema kuwa mchezaji huyo nguli wa soka duniani amekuja Zanzibar  kiutalii kwa ajili ya kuitangaza Zanzibar lakini pia ana azma ya kuifanyia kitu Zanzibar ambacho nikuanzisha kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo kwa vijana wa Zanzibar.

Alieleza kuwa kwa vile maisha yake yote ameitumia katika mchezo wa mpira wa miguu hivyo alisema lazima zawadia mbayo amekuwa nayo kwenye maisha ni kuitunuku  Zanzibar kwa kujenga kituo hicho ambacho kitakuwa  cha kisasa na maalum kwa vijana kuwakuza kimichezo.

Waziri huyo kwa upande wake alieleza utayari wa Serikali kupitia Wizara yake pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo mbali ya kujenga majengo pia, aliahidi kuleta wataalamu wa kutoa mafunzo ya mpira wa miguu kwa vijana.

“Hivyo tunaposema neema tupu sasa tutambue kwamba hizo ndio neema zenyewe tunazozisema”.Alisisitiza Waziri Leila.

Mamadou ambaye ni raia wa Ufaransa amewasili Zanzibar mnamo  Mei 29,2021 kwa ziara ya siku nne akiwa ameambatana na familia yake ambapo tangu alipowasili ameshatembelea Ukanda wa Utalii wa Mashariki, kituo cha kulelea watoto yatima  cha SOS kilichopo Mombasa, Unguja, Mji Mkongwe wa Zanzibar pamoja na kijiji cha Nungwi.

Aidha,  Timu ya Waandishi wa habari wa Televishen ya TF1 ya nchini Ufaransa imefuatana na mchezaji huyo maarufu kwa lengo la kutengeneza makala maalumu ya ziara yake itakayotumika kuutangaza utalii wa Zanzibar kwenye soko la utalii la Ufaransa hususan maeneo yavivutio vya utalii aliyotembelea.

Wanamichezo, wasanii pamoja watu mbalimbali maarufu duniani wamekuwa wakiitembelea Zanzibar mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio vya utalii, ziara hizo za watu mashuhuri ni fursa adhimu ya kuitangaza Zanzibar kiutalii hasa kwa  wale wenye wafuasi wengi katika mitandao yao ya kijamii ambayo ni nyenzo muhimu yenye kufikifiksha ujumbe kwa watu wengi ndani ya muda mfupi.

 Familia yake mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho iliwahi kutembelea Zanzibar mnamo Juni mwaka 2017 wakati huo mchezaji huyo akichezea timu ya Liverpool ya England nakutembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa, Unguja.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar