Na Kassim Abdi, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewaongoza waaumini katika kuusitiri mwili wa Marehemu Wahda Yussuf aliefariki kufuatia ajali ya basi iliotokea Mkoani Shinyanga usiku wa kuamkia Jana iliyojumuisha wanafunzi wengine kutoka Zanzibar.
Mhe. Hemed akiambatana na viongozi wa serikali pamoja na watendaji wa serikali walishiriki katika sala ya maiti iliosaliwa katika Masjid Fatma Kwahani.
Harakati za kuustiri mwili wa marehemu zimefanyika katika makaburi ya waislamu ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.
Makamu wa Pili wa Rais alishiriki katika harakati hizo za mazishi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali katika kusimamia na kugharamia taratibu zote za msiba.
Mapema jana usiku, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, alizifariji Familia za marehemu hao waliofika katika Kiwanja chya ndege cha kimataifa cha Abeid Amani Karume kwa kusema
Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed alizitaka familia hizo kuwa na subira kutokana na msiba huo uliotokea ambao umegusa nyoyo za wananchi wote wa Zanzibar.
Maiti zilizowasili Zanzibar kutokea mkoani Shinyanga ni Rehema Haji Juma aliezikwa Kijijini kwao Kizimukazi
Wahda Yussuf aliezikwa katika makaburi ya mwanakwerekwe na Nassor Juma Khamis aliezikwa Bububu.