NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.
Afisa mdhamini mamlaka ya mapato Tanzania kwa upande wa Pemba Habib Saleh Sultan amesema ushirikiano wa pamoja kati ya TRA masheha na madiwani unahitajika katika kuifikia jamii kwa lengo la kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa wananchi.
Afisa mdhamini huyo amesema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano siku moja kwa madiwani na masheha katika kuwajenga uwelewa juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari huko katika ukumbi wa Baraza la mji Chake Chake..
Amesema tegemeo kubwa la mapato ya taifa ni fedha zitokanazo na kodi kwa wananchi hivyo endapo jamii itapata uwelewa juu ya umuhimu wa ulipaji wa kodi kwa hiari kutasaidia kutimiza malengo ya serikali katika kuwaletea huduma bora wananchi wake na kupiga hatua za maendeleo kwa haraka.
Akifafanua juu ya mamlaka za ulipaji wa kodi kwa upande wa TRA na ZRB Afisa elimu kwa walipa kodi Abdalla Seif amesema vyombo hivyo vya ukusanyaji wa kodi nchini vipo kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.
Akitoa mada katika mkutano huo Afisa elimu na huduma kwa walipa kodi TRA Zanzibar Dr Shuweikha salim khalfan amesema ili Serikali iweze kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa jamii hutumia fedha zitokanazo na kodi za wananchi, hivyo jamii haina budi kufahamu faida za kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi .
Nao washiriki wa mkutano huo wamesema watahakikisha elimu waliopewa wanaifikisha kwa jamii na kuziomba taasisi zinazosimamia kodi kuhakikisha wanasimamia vyema kodi hizo ili ziweze kulipwa kwa wakati.
KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI