Monday, November 25

VIDEO: Wafanyabiashara Kisiwani Pemba waomba kodi zao kutatua kero zinazowakabili.

 

NA KHADIJA KOMBO-PEMBA.

Wafanyabiashara kisiwani Pemba wamesema wao ni wadau wakubwa wa kulipa kodi hivyo ni vyema kodi hizo zikatumika kwa kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili.

Wafanyabiara hao wamesema hayo huko katika ukumbi wa Maktaba Chake Chake wakati walipokuwa  wakichangia katika mafunzo ya kuwasilishaji wa ritani kwa njia ya mtandao.

Wamesema miungoni mwa matatizo yanayowakabili ni miundo mbinu ya bara bara kwani  ni moja kati ya kichocheo kikubwa  katika  kuimarisha biashara zao pamoja na kuleta maendeleo  nchini   lakini bado kwao wao ni kikwazo.

Wakizungumzia juu ya mfumo wa uwasilishaji wa ritani kwa njia ya mtandao  wamesema mfumo huo  utawasaidia kurahisisha kufanya shughuli zao kwa wakati hivyo wameiyomba mamlaka ya mapato kutoa elimu ipasavyo ili waweze kufanya   kazi  hizo   kwa ufanisi zaidi.

Nao maafisa kutoka mamlaka ya mapato Tanzania kwa upande wa Zanzibar wamesema  watahakikisha wanatoa elimu hiyo ipasavyo  ili  walengwa  waweze kuitumia kama ilivyokusudiwa.

KUANGALIA VIDEO BOFYA HAPO CHINI