Tuesday, November 26

Ucheleshwaji wa uendeshwaji kesi za udhalilishaji mahakamani chanzo cha wananchi kushindwa kufika kutoa ushahidi.

NA  FATMA  HAMAD  – PEMBA  .

Ucheleshwaji wa uendeshwaji wa kesi mahakamani ni chanzo kinachochangia baadhi ya wananchi kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi za udhalilishaji hali ambayo inapelekea kesi hizo kushindwa kupata hukumu na hatimae hupelekea kufutwa.

Wakizungumza katika  mkutano wa majadiliano juu ya kupambana na udhalilishaji wa kijinsia, wananchi wa mkoa wa kusini pemba katika mkutano  ambao umewakutanisha watumishi mbali mbali wa Serikali wakiwemo mahakimu, madpp, mapolisi, mafias ustawi wa jamii pamoja na wasaidizi wa sheria huko ukumbi wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Chake chake Pemba.

Wamesema bado uwendeshwaji wa kesi mahakamani unaonekana kusua sua, hivyo hupelekea wazazi wa wahanga  wa matukio ya udhalilishaji kukata tama na kukataa moja kwa moja kwenda mahakamani kutoa ushahidi.

‘’Ukienda leo unaambiwa mjoo, kesho ukija unaambiwa kesho kutwa hii inatuumiza hatuna nauli za kila siku, wakati hata nauli hatupewi  mahakamani ni bora tusamehe tu ‘’Walisema wananchi’’.

Hivyo wamewataka wahusika wa vyombo vya kisheria kuzipa kipaombele kesi hizo na  kuziendesha kwa haraka  ili ziweze kupatiwa huku jambo ambalo litasaidia kuondosha unyama huo ambao umekuwa ni hatari kwa Watoto.

Kaimu mrajis wa mahkama kuu chake chake Abdul Razak Abdul Kadir Ali amesema Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuumwa na tatizo la udhalilishaji imeanzisha mahakama maalu na kuajiri mahakimu 13 Visiwani Zanzibar ambapo kwa pemba kuna makimu wa 5 ambao watashuhulikia kesi hizo  za udhalilishaji tu ili kupunguza malalamiko hayo ya mrundikano wa makesi mahakani.

Kwa upande mwengine Abdul razak amekiri suala la kutokulipwa nauli kwa mashahidi kutokana na ufinyu wa  pesa wanayoletewa kutoka Serikali kuu.

Kwa upande wake mratibu wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Fathiya Mussa Said amesema lengo la mkutano huo ni kujadiliana changamoto mbali mbali katika zinazo wakabili watumishi hao katika ufuatiliaji wa kesi za udhalilishaji.